Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeungana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala katika zoezi la usafi wa mazingira lililofanyika katika eneo la Posta, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya Shirika ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), pamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha mazingira yanakuwa safi, salama na yenye kuvutia. Zoezi hilo, lililoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo, limewakutanisha viongozi na wafanyakazi wa TTCL pamoja na wadau wengine katika kuhamasisha ushiriki wa jamii kwenye shughuli za usafi na utunzaji wa mazingira.
Balozi wa Jamhuri ya Angola nchini Tanzania, Mheshimiwa Domingos Coelho, ametembelea Banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere.
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limetunukiwa tuzo ya kutambua mchango wake mkubwa katika kufanikisha Kongamano la Kwanza la Mwaka la Ulinzi wa Taarifa Binafsi na Faragha, baada ya kudhamini huduma ya intaneti ya uhakika iliyowezesha shughuli zote za kongamano hilo kufanyika kwa ufanisi.
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), kupitia Kitengo cha Uhusiano kwa Umma kutoka Makao Makuu, kwa kushirikiana na watumishi wa TTCL Mkoa wa Dodoma pamoja na kampuni ya Huawei, limefanikisha mafunzo maalum ya huduma bora kwa mteja yaliyolenga timu ya mafundi wanaotoa huduma ya uunganishaji wa intaneti ya Faiba Kwa wateja mbalimbali wa TTCL.
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Agosti 24 mwaka huu lilitoa semina maalum kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Moremi Marwa, amefanya ziara ya kukagua miundombinu mbalimbali ya mawasiliano katika Mkoa wa Pemba ikiwa ni sehemu ya jitihada za Shirika za kuhakikisha uwekezaji uliofanywa katika sekta ya mawasiliano unaleta tija, unaimarisha huduma kwa wananchi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali.
Imeelezwa kuwa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) ni kitovu cha maendeleo ya Sekta ya Mawasiliano na kitovu cha maendeleo ya uchumi wa Kidigitali nchini.
Wananchi na Wadau mbalimbali hususani Wakulima, Wafugaji na Wavuvi wamevutiwa na huduma na bidhaa zinazotolewa na Shirika la mawasiliano Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohammed Khamis Abdulla, amesema
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Jerry William Silaa (Mb) amezindua rasmi Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania - TTCL leo tarehe 16 Desemba, 2024, Makao Makuu ya TTCL, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Balozi Valentino Longino Mlowola, ametembelea banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kuwakaribisha wananchi, wafanyabiashara, taasisi za umma na binafsi kutembelea banda lake lililopo Government Pavilion 2, Viwanja vya John Malecela, Nzuguni jijini Dodoma, ili kujifunza na kujionea kwa karibu huduma na suluhisho mbalimbali za kisasa za mawasiliano na Teknolojia.
Wanafunzi wa Kidato cha Nne kutoka Shule ya Secondari Kinyamwezi wamefanya ziara ya kujifunza masuala mbalimbali
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb),
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Moremi Marwa, amepongeza juhudi za