info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

Latest From Our Blog

News
October 8, 2026 23:57:35 | By Debora Ngalima DKT. NDUMBARO APONGEZA TTCL KWA HUDUMA ZA MAWASILIANO KWA WAJUMBE WA IPU 2026

Mwenyekiti wa Ujumbe wa Tanzania katika Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Damas Ndumbaro (Mb),amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa namna linavyotoa huduma za mawasiliano kwa wajumbe na washiriki wa Mkutano wa IPU 2026 unaofanyika jijini Arusha. Dkt. Ndumbaro alitoa pongezi hizo baada ya kutembelea banda la TTCL katika Mkutano wa IPU 2026, mapema leo Oktoba 8, 2026, ambapo alipata fursa ya kufahamu huduma za mawasiliano zinazotolewa na Shirika hilo kwa ajili ya kuwezesha shughuli za mkutano.

News
October 7, 2026 21:43:52 | By Debora Ngalima IPU 153 YAFUNGUA FURSA ZA KIMKAKATI KWA TTCL KUPITIA MKONGO WA TAIFA

Leo, tarehe 7 Oktoba 2026, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Mbunge wa Jimbo la Uyole na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) anayemaliza muda wake amekutana na Bi. Linda Mushi, akimwakilisha Meneja wa Mkoa wa TTCL Arusha, wakati wa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).

News
October 5, 2026 18:09:20 | By Debora Ngalima TTCL YAUNGANISHA DUNIA ARUSHA, YAWEZESHA MAWASILIANO IPU 2026

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kuonesha uwezo wake katika utoaji wa huduma za mawasiliano ya kisasa baada ya kuwezesha huduma za intaneti na mawasiliano katika Mkutano Mkuu wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), jijini Arusha, kuanzia Oktoba 5 hadi Oktoba 9, 2026.

News
September 29, 2026 08:03:33 | By Debora Ngalima TTCL YAWEZESHA MAWASILIANO YA KIDIJITALI KATIKA KIKAO KAZI CHA WENYEVITI WA BODI NA WAKUU WA TAASISI

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) linaendelea kuonesha nafasi yake muhimu katika kuwezesha shughuli za Serikali kidijitali kwa kutoa huduma ya intaneti yenye uhakika katika Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi (Chairpersons and CEOs Forum) kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina. Kikao hicho kinachofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) kimefunguliwa rasmi leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndenjembi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

News
September 25, 2026 21:18:05 | By Debora Ngalima TTCL YAPANUA FURSA ZA BIASHARA ZA KIDIJITALI, YATUNUKIWA TUZO MKUTANO WA WAHANDISI

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kujitanua katika fursa za biashara za kidijitali baada ya kutunukiwa tuzo ya kutambua mchango wake katika kuwezesha na kufanikisha Mkutano wa 23 wa Wahandisi uliomalizika leo, Septemba 25, 2026, katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

News
September 24, 2026 22:43:30 | By Debora Ngalima WAZIRI ULEGA AIPONGEZA TTCL KWA KUCHOCHEA MAGEUZI YA KIDIJITALI KUPITIA HUDUMA ZA MAWASILIANO

Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Abdallah Ulega (Mb), amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa kuendelea kuwekeza katika huduma za mawasiliano zinazochochea mageuzi ya kidijitali na kurahisisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa wananchi na Taasisi nchini.

Live from Mount Kilimanjaro