info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

Latest From Our Blog

News
August 1, 2026 08:19:53 | By Debora Ngalima TTCL YAENDELEA KUWEKEZA KATIKA KIZAZI KIJACHO CHA WAHANDISI WA MAWASILIANO NCHINI

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kuonesha dhamira yake ya kuwekeza katika maendeleo ya rasilimali watu na kukuza kizazi kijacho cha wataalamu wa mawasiliano nchini kwa kuwapokea wanafunzi kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), waliotembelea Makao Makuu ya Shirika jijini Dar es Salaam kwa mafunzo ya vitendo yaliyofanyika tarehe 30–31 Julai 2026.

News
July 23, 2026 15:29:25 | By Debora Ngalima TTCL YAWAJENGEA UWEZO WANAFUNZI WA DIT KUHUSU UENDESHAJI WA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kukuza ujuzi wa teknolojia nchini kwa kutoa mafunzo ya kitaalamu kwa wanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kuhusu uendeshaji na usimamizi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.

News
July 22, 2026 09:37:17 | By Debora Ngalima KIJA WAJIONEA NGUVU YA TEKNOLOJIA KATIKA KITUO CHA KIDIGITALI KIJITONYAMA

Wanachama wa Kinondoni Jogging Association (KIJA) wametembelea Kituo cha Kidigitali Kijitonyama na kujionea kwa karibu namna teknolojia za kisasa na intaneti yenye kasi zinavyoweza kubadili maisha ya wananchi, kuimarisha biashara na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma mbalimbali.

News
July 20, 2026 15:34:19 | By Debora Ngalima TTCL YAWASHUKURU WATEJA NA WADAU, YAWAKARIBISHA KUENDELEA KUTUMIA HUDUMA ZAKE

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limewashukuru wananchi, wateja na wadau mbalimbali kwa mwitikio mkubwa waliouonesha kwa kutembelea Banda Na. 26 la TTCL katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, maarufu kama Sabasaba. Maonesho hayo yalifanyika kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2026 katika Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam.

News
July 12, 2026 13:50:37 | By Ester Mbanguka WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI TTCL WAJIONEA MAFANIKIO YA HUDUMA NA UBUNIFU WA KIDIJITALI SABASABA 2026

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) watembelea Banda la TTCL katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), ambapo wamejionea maendeleo ya huduma na suluhisho mbalimbali za kidijitali zinazotolewa na Shirika kwa wananchi, taasisi za umma, sekta binafsi na wafanyabiashara.

News
July 11, 2026 17:00:16 | By Ester Mbanguka MWENYEKITI WA BODI YA UCSAF AVUTIWA NA UBUNIFU WA TTCL SABASABA 2026

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Balozi Valentino Longino Mlowola, ametembelea banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Live from Mount Kilimanjaro