Wanachama wa Kinondoni Jogging Association (KIJA) wametembelea Kituo cha Kidigitali Kijitonyama na kujionea kwa karibu namna teknolojia za kisasa na intaneti yenye kasi zinavyoweza kubadili maisha ya wananchi, kuimarisha biashara na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma mbalimbali.
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limewashukuru wananchi, wateja na wadau mbalimbali kwa mwitikio mkubwa waliouonesha kwa kutembelea Banda Na. 26 la TTCL katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, maarufu kama Sabasaba. Maonesho hayo yalifanyika kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2026 katika Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) watembelea Banda la TTCL katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), ambapo wamejionea maendeleo ya huduma na suluhisho mbalimbali za kidijitali zinazotolewa na Shirika kwa wananchi, taasisi za umma, sekta binafsi na wafanyabiashara.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Balozi Valentino Longino Mlowola, ametembelea banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL-PESA Bw. Richard Mayongela akiongozana na Wajumbe wengine wametembelea Banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), ambapo walijionea huduma mbalimbali za kidijitali na suluhisho za kifedha zinazotolewa kupitia T-PESA kwa wananchi, taasisi na wafanyabiashara.
Maafisa wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wanaendelea kuwahudumia wananchi wanaotembelea Banda la TTCL katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), kwa kuwapatia elimu kuhusu huduma na suluhisho mbalimbali za mawasiliano na teknolojia za kidijitali zinazotolewa na TTCL.