Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kujitanua katika fursa za biashara za kidijitali baada ya kutunukiwa tuzo ya kutambua mchango wake katika kuwezesha na kufanikisha Mkutano wa 23 wa Wahandisi uliomalizika leo, Septemba 25, 2026, katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Abdallah Ulega (Mb), amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa kuendelea kuwekeza katika huduma za mawasiliano zinazochochea mageuzi ya kidijitali na kurahisisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa wananchi na Taasisi nchini.
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo limefanya kipindi maalum kupitia Radio Uhuru FM, kwa lengo la kuwafikishia wananchi elimu kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Shirika pamoja na fursa zinazopatikana kupitia teknolojia ya mawasiliano.
Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Bw. Vedastus Mwita ameshiriki katika kipindi cha Baragumu Live cha televisheni kupitia Channel Ten na kueleza hatua mbalimbali zinazotekelezwa na Shirika katika kuimarisha na kupanua huduma za mawasiliano ya kidijitali nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Moremi Marwa, amefanya ziara mkoani Kigoma kwa lengo la kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya mawasiliano, inayolenga kuimarisha miundombinu ya kidijitali, kuongeza upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kufungua fursa mpya za biashara ndani na nje ya Tanzania.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Kairuki, amewataka Watanzania kuchangamkia fursa zinazotokana na huduma za mawasiliano zinazotolewa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), hususan huduma za intaneti ya kasi kupitia Faiba Mlangoni Kwako, ili kuongeza matumizi ya teknolojia katika shughuli za kila siku na kuchangia ukuaji wa uchumi wa kidijitali nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe. Salum Abdalah Kalli, amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa mchango wake katika kuimarisha sekta ya mawasiliano nchini na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na za uhakika, ikiwemo huduma ya intaneti kupitia Faiba Mlangoni Kwako.
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB), na Burundi Backbone System (BBS) wamesaini mkataba wa kuongeza uwezo wa huduma za mawasiliano nchini Burundi kutoka 4Gbps hadi 10Gbps.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mhe. Dkt. Riziki Pembe Juma, amesema ushirikiano kati ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) una fursa kubwa ya kubadilisha uendeshaji wa soka Zanzibar kwa kutumia teknolojia za kidijitali.
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), kupitia Kitengo cha Uhusiano kwa Umma kutoka Makao Makuu, kwa kushirikiana na watumishi wa TTCL Mkoa wa Dodoma pamoja na kampuni ya Huawei, limefanikisha mafunzo maalum ya huduma bora kwa mteja yaliyolenga timu ya mafundi wanaotoa huduma ya uunganishaji wa intaneti ya Faiba Kwa wateja mbalimbali wa TTCL.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewakamata watu 11 wanaodaiwa kujihusisha na wizi, uharibifu, usafirishaji na biashara ya miundombinu ya mawasiliano ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), huku likisema hali ya usalama jijini kwa ujumla ni shwari.
Kampuni Tanzu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), T-PESA, kupitia huduma yake ya N-card, imeendelea kudhihirisha dhamira yake ya kuunga mkono maendeleo ya soka Zanzibar kwa kudhamini na kushiriki kikamilifu katika Mchezo wa Ngao ya Jamii 2026 uliozikutanisha KVZ FC na KMKM SC uliofanyika tarehe 23 Agosti 2026 katika Uwanja wa Mao, Zanzibar.
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kwa kushirikiana na wadau, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uhusiano na jamii, kuhamasisha matumizi ya teknolojia katika maisha ya kila siku. Katika kuunga mkono juhudi hizo, TTCL imeshiriki Tamasha la Kinondoni Jogging Association (KIJA) 2026, lililofanyika Viwanja Vya Posta Kijitonyama likilenga kuwakutanisha wananchi katika shughuli za kijamii, afya na burudani.
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limezindua rasmi utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mradi wa Faiba Mlangoni Kwako (FTTH), hatua inayolenga kuongeza upatikanaji wa huduma ya intaneti ya kasi kwa wananchi, taasisi za umma na binafsi pamoja na wafanyabiashara kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. Uzinduzi wa mradi huo umefanyika leo, Agosti 21, 2026, katika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb).
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kujenga mazingira wezeshi kwa uchumi wa kidijitali Zanzibar kwa kuwezesha huduma ya intaneti katika mradi wa makazi wa Amani Residency, uliopo Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, kupitia huduma yake ya Faiba Mlangoni Kwako.