info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100
Habari
July 1, 2026 22:40:31 | Na Ester Mbanguka NAIBU GAVANA WA BENKI KUU ATEMBELEA BANDA LA TTCL SABASABA 2026, APONGEZA MAGEUZI YA KIDIJITALI

TTCL tunamshukuru Naibu Gavana wa Benki Kuu kwa kutembelea banda letu na kwa kutambua mchango wa Shirika katika kujenga Tanzania ya kidijitali.

Habari
July 1, 2026 18:59:44 | Na Ester Mbanguka TTCL YAENDELEA KUTOA HUDUMA NA ELIMU KWA WANANCHI SABASABA 2026

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) linaendelea kutumia Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026) kutoa huduma na elimu kwa wananchi kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali za mawasiliano zinazotolewa na Shirika hilo.

Habari
June 30, 2026 19:34:51 | Na Ester Mbanguka TTCL YAANDIKA HISTORIA, YATUNUKIWA TUZO NA RAIS SAMIA BAADA YA KUREJEA KWENYE FAIDA

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeandika historia mpya baada ya kutunukiwa Tuzo Maalum na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia mafanikio ya kurejea kwenye faida kwa mara ya kwanza baada ya kipindi kirefu cha changamoto za kifedha.

Habari
June 29, 2026 23:12:55 | Na Ester Mbanguka TTCL YAJIPANGA KIKAMILIFU KUWAHUDUMIA WATEJA SABASABA 2026

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limejipanga kikamilifu kuhakikisha wateja na wananchi wanaotembelea Banda Na. 26 katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026) wanapata huduma bora, elimu kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali za kidijitali, pamoja na suluhisho zinazokidhi mahitaji yao.

Habari
June 29, 2026 22:37:01 | Na Ester Mbanguka TTCL YADHAMINI HUDUMA YA INTANETI KATIKA KONGAMANO LA KWANZA LA KITAIFA LA FARAGHA NA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI 2026

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Switbert Zacharia Mkama (Mb), amefungua rasmi Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Faragha na Ulinzi wa Taarifa Binafsi 2026, linalofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, kuanzia Juni 29 hadi Julai 1, 2026.

Habari
June 28, 2026 18:39:47 | Na Ester Mbanguka TTCL YASHIRIKI MAONESHO YA 50 YA BIASHARA YA KIMATAIFA SABASABA 2026

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) linashiriki katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Habari
June 24, 2026 09:28:13 | Na Ester Mbanguka “TTCL NI MHIMILI MUHIMU KUELEKEA TANZANIA YA KIDIJITALI" – PROFESA SHEMDOE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe Profesa Riziki Shemdoe ametoa rai kwa wananchi kutumia huduma zinazotolewa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) huku akipongeza juhudi za Shirika hilo katika kutekeleza dhamira ya Serikali ya kujenga Tanzania ya kidijitali na kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora na za uhakika za mawasiliano.

Habari
June 23, 2026 10:28:50 | Na Ester Mbanguka TTCL YAPONGEZWA KWA KUUNGA MKONO AJENDA YA TANZANIA YA KIDIJITALI

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Afya), Mhe. Dkt. Jafar Rajab Seif, amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa mchango wake katika kuimarisha miundombinu ya mawasiliano na kuunga mkono jitihada za Serikali za kujenga uchumi wa kidijitali kupitia utoaji wa huduma za kisasa za TEHAMA.

Habari
June 23, 2026 10:24:03 | Na Ester Mbanguka MHE. HALIMA DENDEGO AHAMASISHA MATUMIZI YA HUDUMA ZA TTCL

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, amewahimiza wananchi, taasisi za umma na binafsi pamoja na wafanyabiashara kuendelea kutumia huduma zinazotolewa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), akieleza kuwa Shirika hilo lina mchango mkubwa katika kuimarisha sekta ya mawasiliano na kuharakisha maendeleo ya uchumi wa kidijitali nchini.

Habari
June 17, 2026 17:26:40 | Na Ester Mbanguka WATUMISHI WAHIMIZWA KUIMARISHA UWAJIBIKAJI KWA HUDUMA ENDELEVU KWA WANANCHI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb), amezindua rasmi Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2026 yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma, huku akiwataka watumishi wa umma nchini kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uwajibikaji na kujituma katika kutoa huduma bora na endelevu kwa wananchi.

Habari
June 16, 2026 17:14:06 | Na Ester Mbanguka TTCL YASHIRIKI MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2026 DODOMA

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) linashiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2026 yanayofanyika kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni 2026 katika Viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma.

Habari
June 11, 2026 17:38:11 | Na Ester Mbanguka MKURUGENZI MKUU WA TTCL AKAGUA MIUNDOMBINU YA MAWASILIANO NA MIRADI YA UPANUZI WA FAIBA PEMBA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Moremi Marwa, amefanya ziara ya kukagua miundombinu mbalimbali ya mawasiliano katika Mkoa wa Pemba ikiwa ni sehemu ya jitihada za Shirika za kuhakikisha uwekezaji uliofanywa katika sekta ya mawasiliano unaleta tija, unaimarisha huduma kwa wananchi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali.

Habari
June 11, 2026 17:32:18 | Na Ester Mbanguka TTCL YAONGEZA KASI YA UPANUZI WA HUDUMA ZA FAIBA ARUSHA, MKURUGENZI MKUU AKAGUA MAENDELEO

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Moremi Marwa, amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya utoaji wa huduma ya intaneti yenye kasi ya TTCL Faiba katika makazi ya wananchi jijini Arusha, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Shirika za kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora, za uhakika na zenye kukidhi mahitaji ya uchumi wa kidijitali.

Habari
June 4, 2026 17:32:16 | Na Ester Mbanguka UJUMBE WA UETCL WAPONGEZA TTCL KWA KUKUZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA KIDIJITALI AFRIKA MASHARIKI

Ujumbe kutoka Kampuni ya Kusafirisha Umeme nchini Uganda (Uganda Electricity Transmission Company Limited - UETCL) umetembelea Kijitonyama FTTx Experience Centre na kupongeza juhudi za Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika kuwekeza kwenye miundombinu na suluhisho za kidijitali zinazochangia maendeleo ya sekta ya mawasiliano nchini Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki.

Habari
June 4, 2026 17:29:37 | Na Ester Mbanguka WAFANYAKAZI WA TTCL MKOA WA PWANI WAJENGEWA UWEZO KUHUSU TEKNOLOJIA ZA FTTX

Wafanyakazi wa TTCL Mkoa wa Pwani, wakiongozwa na Meneja wa Mkoa, Bw. Abdulrahim Chotta, wametembelea Kijitonyama FTTx Experience Centre kwa lengo la kujifunza, kubadilishana uzoefu na kuongeza uelewa kuhusu teknolojia za kisasa za mawasiliano zinazotolewa na Shirika.