Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), limeshiriki Mbio za CRDB International Marathon Msimu wa Nne ambapo ambapo zililenga kukusanya fedha kwa ajili ya kuwasaidia Wanawake wenye ugonjwa wa Fistula wanaotibiwa katika Hospitali ya CCBRT Jijini Dar es Salaam.
Wananchi na Wadau mbalimbali hususani Wakulima, Wafugaji na Wavuvi wamevutiwa na huduma na bidhaa zinazotolewa na Shirika la mawasiliano Tanzania.
Waziri wa Kilimo. Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Mhe. Shamata Khamis amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania –TTCL kwa huduma wanazozitoa ambapo zimerahisisha Mawasiliano Nchini Tanzania na nje ya Nchi.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) awatunuku tuzo na vyeti kwa washiriki 57 walioshiriki katika uzinduzi wa huduma ya mawasiliano Intaneti katika kilele cha Mlima Kilimanjaro Disemba 13, 2022.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akabidhi tuzo kwa familia ya Marehemu Joachim Kapembe, kwa kutambua na kuthamini mchango wa Marehemu Joachim Kapembe wakati wa uzinduzi wa huduma ya Mawasiliano ya Intaneti katika kilele cha Mlima Kilimanjaro Disemba 13 2022.
Wafanyakazi 14 wa TTCL na KINAPA watunukiwa tuzo maalum kwa kufanikisha ujenzi wa mawasiliano ya Intaneti katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) ametembelea banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania -TTCL lililopo ndani ya TEHAMA PAVILION katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kampuni Tanzu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL ya T-PESA imezindua huduma mpya ya kifedha ya Akaunti Pepe(Virtual Account) ambayo inamuwezesha mtumiaji kufanya miamala ya kifedha kwa usalama na hivyo kuongeza chachu katika kukuza matumizi ya kifedha kidijitali.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano la Tanzania- TTCL Bi. Zuhura Muro amesema TTCL inauwezo wa kuifanya Tanzania kuwa nchi kiongozi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC kutokana uwepo wa miundombinu bora ya mawasiliano yenye uwezo wa kufanikisha ukuaji wa uchumi wa kidjitali.
Tarehe 8 Machi kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Wanawake, ama Siku ya Wanawake Duniani. Katika siku hii, wanawake wa Shirika la Mawasiliano Tanzania huungana na Wanawake wenzao duniani kote kuadhimisha siku hii muhimu.