info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

Malengo Makuu ya Biashara

Mabadiliko ya Biashara ya TTCL yanalenga mageuzi ya uwezo wa utoaji huduma za sauti na data kwa kutumia teknolojia iliyoboreshwa na maarufu zaidi katika soko la sasa.

Kwa hivyo, SBP itazingatia uwekaji wa 4G- LTE , Wi-Fi, FTTx, na GSM - 2G,3G kwa ajili ya kutoa huduma za broadband na simu katika ubora wa juu. Kwa mara ya kwanza katika soko la mawasiliano ya simu, TTCL ikiwa na fursa za kuwa na miundombinu ya mtandao wa laini zisizobadilika, kampuni ilipanga kutoa huduma zilizounganishwa kupitia Fixed Mobile Convergence (FMC).

Kwa mtandao wa LTE, TTCL itaweza kuhifadhi na kukuza wateja wake wa broadband na kupata mapato kwa viwango vya gharama endelevu. Wakati huo huo, TTCL itaendelea kutumia faida yake iliyopo ya ushindani kwenye huduma za mkongo wa jumla (carrier of carriers) na huduma za broadband zisizobadilika huku ikizingatia matumizi bora ya rasilimali za ndani na nje katika utoaji wa huduma na uwekezaji kwa upanuzi mkubwa wa mtandao.

Chini ya mpango mkakati huu wa mabadiliko ya biashara, TTCL itatoa:

  • GSM – 2G na UMTS- 3G inaenea kote nchini.
  • LTE-4G inaenea miji mikubwa,
  • Huduma za Ongezeko la Thamani,
  • Huduma za Mobile Money, malipo ya kutuma na kupokea pesa, kulipa bili n.k.

Mabadiliko ya biashara ya TTCL yanakwenda sambamba na uboreshaji wa utoaji huduma (QoS) kwa Wateja wa Makampuni, Wadogo na wa kati na makazi.