info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100
Habari
August 21, 2026 19:07:11 | Na Debora Ngalima TTCL YAZINDUA FAIBA MLANGONI KWAKO AWAMU YA PILI, WATEJA 400,000 KUNUFAIKA

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limezindua rasmi utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mradi wa Faiba Mlangoni Kwako (FTTH), hatua inayolenga kuongeza upatikanaji wa huduma ya intaneti ya kasi kwa wananchi, taasisi za umma na binafsi pamoja na wafanyabiashara kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. Uzinduzi wa mradi huo umefanyika leo, Agosti 21, 2026, katika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb).

Habari
August 17, 2026 14:58:58 | Na Debora Ngalima TTCL YAWEZESHA INTANETI YA KASI KATIKA MAKAZI YA AMANI RESIDENCY ZANZIBAR

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kujenga mazingira wezeshi kwa uchumi wa kidijitali Zanzibar kwa kuwezesha huduma ya intaneti katika mradi wa makazi wa Amani Residency, uliopo Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, kupitia huduma yake ya Faiba Mlangoni Kwako.

Habari
August 17, 2026 14:48:48 | Na Debora Ngalima TTCL YAIBUKA KINARA WA HUDUMA BORA ZA MAWASILIANO NCHINI

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limetajwa kuwa kinara katika utoaji wa huduma bora za mawasiliano nchini, hatua inayothibitisha mafanikio ya uwekezaji wa muda mrefu katika miundombinu na mifumo ya huduma kwa wateja.

Habari
August 17, 2026 14:42:45 | Na Debora Ngalima TTCL YATUNUKIWA CHETI CHA SHUKRANI KIZIMKAZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemkabidhi cheti Meneja TTC Zanzibar Bi. Nasra Mugheiry , ishara ya kutambua mchango wa Shirika la Mawasiliano (TTCL) katika kudhamini, kushiriki na kuunga mkono Tamasha la Kizimkazi ambalo lilifikia kilele Agosti 14, 2026 Kizimkazi, Kusini Unguja, Zanzibar.

Habari
August 14, 2026 16:30:38 | Na Debora Ngalima KIZIMKAZI 2026 YAFIKIA KILELE LEO ZANZIBAR, MHE. RAIS AFUNGA RASMI

Tamasha la Kizimkazi 2026 limefikia kilele chake leo katika Viwanja vya Makunduchi, Zanzibar, likihudhuriwa na kufungwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Habari
August 14, 2026 16:19:54 | Na Debora Ngalima MHE. RAIS APITA BANDA LA TTCL, AWASALIMIA VIONGOZI NA WAFANYAKAZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasalimia Viongozi na Wafanyakazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) waliokuwa wakiliwakilisha Shirika katika banda la maonesho wakati wa Tamasha la Kizimkazi 2026.

Habari
August 14, 2026 16:16:59 | Na Debora Ngalima NAIBU WAZIRI MHE. WANU HAFIDH AMEIR ATEMBELEA BANDA LA TTCL KIZIMKAZI 2026

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa Makunduchi, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, ametembelea banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika Maonesho ya Tamasha la Kizimkazi 2026, Zanzibar.

Habari
August 12, 2026 16:32:47 | Na Debora Ngalima RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA TTCL KIZIMKAZI.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametembelea Banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika Maonesho ya Tamasha la Kizimkazi 2026, ambapo amepata fursa ya kufahamu huduma na mchango wa TTCL katika kuimarisha mawasiliano na kuchochea maendeleo ya uchumi wa kidijitali Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Habari
August 12, 2026 14:26:03 | Na Debora Ngalima TTCL YAENDELEA KUTOA FURSA YA MAFUNZO KWA VITENDO KWA WANAFUNZI KUTOKA VYUO MBALIMBALI NCHINI

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kutekeleza wajibu wake wa kijamii na kitaifa kwa kuwapokea wanafunzi kutoka vyuo na kada mbalimbali nchini kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo (Field Attachment) kwa mwaka wa masomo 2026/2027.

Habari
August 7, 2026 11:29:05 | Na Debora Ngalima TTCL YAWAKARIBISHA WANANCHI KUJIONEA NGUVU YA MAWASILIANO KATIKA MAONESHO YA NANENANE DODOMA

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kuwakaribisha wananchi, wafanyabiashara, taasisi za umma na binafsi kutembelea banda lake lililopo Government Pavilion 2, Viwanja vya John Malecela, Nzuguni jijini Dodoma, ili kujifunza na kujionea kwa karibu huduma na suluhisho mbalimbali za kisasa za mawasiliano na Teknolojia.

Habari
August 6, 2026 23:16:58 | Na Debora Ngalima TANZANIA YAFUATILIA TEKNOLOJIA ZA JUU ZA KIDIGITALI NCHINI VIETNAM

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb), akiambatana na ujumbe kutoka Tanzania ikiwemo Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Moremi Marwa wamefanya ziara Viettel High Technology Industries jijini Hanoi, Vietnam.

Habari
August 5, 2026 11:38:38 | Na Debora Ngalima TTCL INAENDELEA KUTOA HUDUMA NA ELIMU KWA WAKULIMA NA WANANCHI NANENANE 2026

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) linaendelea kutoa huduma na elimu kwa wakulima na wananchi wanaotembelea Maonesho ya Nanenane 2026 yanayofanyika katika Uwanja wa John Malecela Nzuguni, jijini Dodoma.

Habari
August 4, 2026 17:50:04 | Na Debora Ngalima TTCL YAJA NA OFA KABAMBE MSIMU WA MAONESHO YA NANE NANE 2026

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limetangaza ofa kabambe ya punguzo la bei kwenye vifaa vya intaneti kwa wananchi wanaotembelea banda lake katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nane Nane 2026, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha matumizi ya teknolojia ya kidijitali na kuongeza upatikanaji wa huduma bora za mawasiliano nchini.

Habari
August 1, 2026 08:19:53 | Na Debora Ngalima TTCL YAENDELEA KUWEKEZA KATIKA KIZAZI KIJACHO CHA WAHANDISI WA MAWASILIANO NCHINI

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kuonesha dhamira yake ya kuwekeza katika maendeleo ya rasilimali watu na kukuza kizazi kijacho cha wataalamu wa mawasiliano nchini kwa kuwapokea wanafunzi kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), waliotembelea Makao Makuu ya Shirika jijini Dar es Salaam kwa mafunzo ya vitendo yaliyofanyika tarehe 30–31 Julai 2026.

Habari
July 23, 2026 15:29:25 | Na Debora Ngalima TTCL YAWAJENGEA UWEZO WANAFUNZI WA DIT KUHUSU UENDESHAJI WA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kukuza ujuzi wa teknolojia nchini kwa kutoa mafunzo ya kitaalamu kwa wanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kuhusu uendeshaji na usimamizi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.