info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

TUMIENI MAWASILIANO KWA USTAWI WA MIFUGO NA KILIMO

Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL limetoa rai kwa wakulima kutumia huduma ya mtandao ili kuboresha kilimo lakini pia kuendana na teknolojia.

Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Afisa Uhusiano TTCL Ester Mbanguka wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Wakulima Nane Nane katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Alisema katika maonesho hayo shirika lilitoa huduma mbalimbali ambazo zililenga kuwasaidia wakulima na Wafugaji hasa wanaofanya shughuli zao kwa njia ya kisasa ambapo huduma ya mawasalino inayotolewa na shirika hilo ni imara inalenga kurahisisha shughuli mbalimbali ikiwemo ufugaji na kilimo kufanyika kidigitali ikiwa ni pamoja na  kufuatilia masoko, kupata taarifa za hali ya hewa na mafunzo kuhusu mazao na mifugo.

Aidha aliongeza kuwa katika maonesho hayo shirika lilipata wateja wa huduma ya internet ambao ni washiriki wa maonesho hayo ambapo pia shirika hilo lilitoa huduma ya  interneti ya bure ili kuwawezesha Wananchi na washiriki kutoka Sekta mbalimbali zinazoshiriki katika maonesho hayo kufanya shughuli zao kwa haraka na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kipindi chote cha maonesho.

Katika hatua nyingine Ester amewataka wateja wa TTCL kote nchini kutoa taarifa kituo cha huduma kwa wateja pindi wanapopata changamoto yoyote pindi wanapotumia huduma na bidhaa za shirika hilo ili ziweze kutatuliwa kwa wakati.

 

 

 

.