BANDA LA TTCL LAWA KIVUTIO KILELE CHA NANENANE MBEYA
Wananchi na Wadau mbalimbali hususani Wakulima, Wafugaji na Wavuvi wamevutiwa na huduma na bidhaa zinazotolewa na Shirika la mawasiliano Tanzania. Wakiwa katika banda la shirika hilo wakati wa kilele cha Maonesho ya Siku Kuu ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nanenane) wamepata fursa ya kujifunza jinsi Shirika linavyotoa huduma zake ikiwemo Faiba Mlangoni ambayo huduma ya intaneti yenye kasi zaidi. Wamesema huduma hii ni nzuri kwani pamoja na mambo mengine itawarahisishia kupata taarifa za hali ya hewa, kujua masoko na hivyo kuwa chachu katika ukuaji wa uchumi nchini. Katika hatua nyingine wametoa pongezi kwa TTCL kwa jitihada zake za kufanikisha kufikisha huduma ya intaneti katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro. Mbali na kutoa pongezi pia wametoa rai kwa Watumishi wa shirika hilo kuendelea kuchapa kazi ili kuhakikisha mawasiliano pamoja na fursa mbalimbali zilizopo sekta ya mawasiliano zinawafikia Wananchi wote ili kuwaongezea kipato. Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi yamehitimishwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Agosti 8 mwaka huu.