info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

MIUNDOMBINU BORA YA MAWASILIANO KITOVU CHA UKUAJI UCHUMI KIDIGITALI

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano la Tanzania- TTCL Bi. Zuhura Muro amesema TTCL inauwezo wa kuifanya Tanzania kuwa nchi kiongozi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC kutokana uwepo wa miundombinu bora ya mawasiliano yenye uwezo wa kufanikisha ukuaji wa uchumi wa kidjitali.

 Bi. Zuhura alizungumza hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea banda la TTCL katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam,alisema anaaamini kuwa Shirika hili likiendelea kufanya vizuri katika mawanda ya uchumi wa kidjitali kwa Tanzania utazidi kupanda kwa kasi ya juu.

 Amesema kutokana na dunia ya sasa ipo kidjitali ndio maana TTCL hadi sasa imepiga hatua katika kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kutumia magari kutangaza utalii hali iliyofanya watanzania kwa sasa kuona picha mubashara ya watalii wakipanda mlima wa Kilimanjaro na kuona hali yake.

 “Kwa hatua kubwa TTCL imepiga hatua kubwa sana kwa nguvu walizoweka hasa katika Mkongo ni kuunganisha nchi kila kona na katika kuunganisha nchi yetu itakuwa na maingiliano ya tija zaidi na kuwezesha uchumi wetu kwenda mbele zaidi,”amesema. 

Aidha amesema nchi itakapounganisha nchi nyingine kidigitali itaweza kusaidia kuongeza pato la mapato ya fedha za kigeni na uchumi kuzidi kukua.”Nimepata fursa ya kutembelea banda letu leo na nimefurahi sana kutokana na unyeti wa Shirika hili kwa taifa letu hasa wanapozungumzia uchumi wa kidjitali,”alisema na kuongeza “Tutauza ubunifu, Teknolojia nje ya nchi kupitia TTCL huku Watanzania wataona jinsi ambavyo shirika linavyonda na uwezo wa kuifanya Tanzania ikawa nchi kiongozi siyo tu kiteknolojia lakini kiuchumi katika ukanda wetu ,kiusalama na kiutamanduni pindi itakapouza digitali,”amesema.

Amesema kukuza huduma za kidigitali ni maendeleo yaliyopo katika Shirika hilo kwani shirika linaweza kuwa muhimili mkubwa katika kuhifadhi data za wafanyabiashara hata wale wa kati ambapo data zitakuwa salama.