info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

IMARISHENI MIUNDOMBINU YA MAWASILIANO ILI KUFIKIA MALENGO YA SERIKALI – MHANDISI MAHUNDI

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb), hivi karibuni alifanya ziara ya kikazi katika Kituo cha Mkongo wa Taifa cha Kibaha, Kituo cha Mkongo wa Taifa Chalinze na kutembelea Mnara wa mawasiliano uliopo Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere Kibaha, mkoani Pwani.

Mhe. Mhandisi Mahundi alifanya ziara hiyo ikiwa ni sehemu ya kufuatilia utekelezaji wa miradi ya mbalimbali ya mawasiliano nchini.

Aidha ziara hiyo ilikuwa na lengo la kuhakikisha maendeleo ya sekta ya mawasiliano yanawiana na matarajio ya Serikali kwakuzingatia mahitaji ya wananchi.

Katika ziara hiyo, Mhe. Mhandisi Mahundi alijionea miundombinu ya Mkongo wa Taifa na mnara wa mawasiliano na kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayolenga kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasiliano nchini. 

Mhe. Mhandisi Mahundi alisisitiza umuhimu wa kuimarisha miundombinu hiyo ili kufanikisha lengo la serikali la kuhakikisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa gharama nafuu na zinazowafikia wananchi wengi zaidi.