info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

T-PESA YATOA ELIMU YA MIAMALA TAMASHA LA FINTECH

 

T-PESA Kampuni tanzu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) imeendelea kutoa elimu ya miamala salama ya fedha kimtandao kwa wananchi mbalimbali waliotembelea banda la T-Pesa katika Tamasha la Teknolojia la Fedha 2025 (Fintech festival 2025) lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa JNICC Jijini Dar es salaam.

Katika tamasha hilo T-Pesa kupitia Wataalam wake imeendelea kutoa elimu kuhusu matumizi salama ya fedha kidijitali, mifumo ya malipo salama, usalama wa miamala na matumizi bora ya huduma za kifedha mtandaoni.

Pia T-Pesa inatoa fursa kwa wananchi kujifunza na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni hiyo zikiwemo, huduma za kutuma na kupokea fedha, malipo ya huduma mbalimbali za kijamii kwa kutumia N-card na huduma za kifedha nyinginezo kupitia simu za mkononi.

Lengo la T-Pesa kutoa elimu hii ni kuwajengea uelewa wananchi juu ya huduma zinazotolewa na na kampuni hiyo ili kuwawezesha wananchi kutumia huduma za kifedha kidijitali ambayo ni njia salama, nafuu na yenye ufanisi zaidi.

Tamasha la Teknolojia la Fedha la Mwaka 2025 lilianza Juni 12 hadi 13 Juni mwaka huu 2025, liliwakutanisha washiriki kutoka nchi 56 za Afrika ikiwemo Tanzania, ambapo linawaleta pamoja Wabunifu, Wajasiriamali na Wataalamu kutoka Sekta ya Fedha na Teknolojia ili kujadili maendeleo ya kiteknolojia katika sekta ya fedha barani Afrika huku likijadili kwa kina mustakabali wa huduma za kifedha na mabadiliko ya kidijitali katika nchi za Kiafrika.