info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100
News
August 7, 2026 11:29:05 | By Debora Ngalima TTCL YAWAKARIBISHA WANANCHI KUJIONEA NGUVU YA MAWASILIANO KATIKA MAONESHO YA NANENANE DODOMA

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kuwakaribisha wananchi, wafanyabiashara, taasisi za umma na binafsi kutembelea banda lake lililopo Government Pavilion 2, Viwanja vya John Malecela, Nzuguni jijini Dodoma, ili kujifunza na kujionea kwa karibu huduma na suluhisho mbalimbali za kisasa za mawasiliano na Teknolojia.

News
August 6, 2026 23:16:58 | By Debora Ngalima TANZANIA YAFUATILIA TEKNOLOJIA ZA JUU ZA KIDIGITALI NCHINI VIETNAM

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb), akiambatana na ujumbe kutoka Tanzania ikiwemo Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Moremi Marwa wamefanya ziara Viettel High Technology Industries jijini Hanoi, Vietnam.

News
August 5, 2026 11:38:38 | By Debora Ngalima TTCL INAENDELEA KUTOA HUDUMA NA ELIMU KWA WAKULIMA NA WANANCHI NANENANE 2026

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) linaendelea kutoa huduma na elimu kwa wakulima na wananchi wanaotembelea Maonesho ya Nanenane 2026 yanayofanyika katika Uwanja wa John Malecela Nzuguni, jijini Dodoma.

News
August 4, 2026 17:50:04 | By Debora Ngalima TTCL YAJA NA OFA KABAMBE MSIMU WA MAONESHO YA NANE NANE 2026

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limetangaza ofa kabambe ya punguzo la bei kwenye vifaa vya intaneti kwa wananchi wanaotembelea banda lake katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nane Nane 2026, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha matumizi ya teknolojia ya kidijitali na kuongeza upatikanaji wa huduma bora za mawasiliano nchini.

News
August 1, 2026 08:19:53 | By Debora Ngalima TTCL YAENDELEA KUWEKEZA KATIKA KIZAZI KIJACHO CHA WAHANDISI WA MAWASILIANO NCHINI

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kuonesha dhamira yake ya kuwekeza katika maendeleo ya rasilimali watu na kukuza kizazi kijacho cha wataalamu wa mawasiliano nchini kwa kuwapokea wanafunzi kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), waliotembelea Makao Makuu ya Shirika jijini Dar es Salaam kwa mafunzo ya vitendo yaliyofanyika tarehe 30–31 Julai 2026.

News
July 23, 2026 15:29:25 | By Debora Ngalima TTCL YAWAJENGEA UWEZO WANAFUNZI WA DIT KUHUSU UENDESHAJI WA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kukuza ujuzi wa teknolojia nchini kwa kutoa mafunzo ya kitaalamu kwa wanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kuhusu uendeshaji na usimamizi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.

News
July 22, 2026 09:37:17 | By Debora Ngalima KIJA WAJIONEA NGUVU YA TEKNOLOJIA KATIKA KITUO CHA KIDIGITALI KIJITONYAMA

Wanachama wa Kinondoni Jogging Association (KIJA) wametembelea Kituo cha Kidigitali Kijitonyama na kujionea kwa karibu namna teknolojia za kisasa na intaneti yenye kasi zinavyoweza kubadili maisha ya wananchi, kuimarisha biashara na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma mbalimbali.

News
July 20, 2026 15:34:19 | By Debora Ngalima TTCL YAWASHUKURU WATEJA NA WADAU, YAWAKARIBISHA KUENDELEA KUTUMIA HUDUMA ZAKE

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limewashukuru wananchi, wateja na wadau mbalimbali kwa mwitikio mkubwa waliouonesha kwa kutembelea Banda Na. 26 la TTCL katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, maarufu kama Sabasaba. Maonesho hayo yalifanyika kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2026 katika Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam.

News
July 12, 2026 13:50:37 | By Ester Mbanguka WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI TTCL WAJIONEA MAFANIKIO YA HUDUMA NA UBUNIFU WA KIDIJITALI SABASABA 2026

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) watembelea Banda la TTCL katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), ambapo wamejionea maendeleo ya huduma na suluhisho mbalimbali za kidijitali zinazotolewa na Shirika kwa wananchi, taasisi za umma, sekta binafsi na wafanyabiashara.

News
July 11, 2026 17:00:16 | By Ester Mbanguka MWENYEKITI WA BODI YA UCSAF AVUTIWA NA UBUNIFU WA TTCL SABASABA 2026

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Balozi Valentino Longino Mlowola, ametembelea banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

News
July 7, 2026 13:29:31 | By Ester Mbanguka VIONGOZI WA BODI YA T-PESA WATEMBELEA BANDA LA TTCL SABASABA 2026

Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL-PESA Bw. Richard Mayongela akiongozana na Wajumbe wengine wametembelea Banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), ambapo walijionea huduma mbalimbali za kidijitali na suluhisho za kifedha zinazotolewa kupitia T-PESA kwa wananchi, taasisi na wafanyabiashara.

News
July 6, 2026 22:34:07 | By Ester Mbanguka WANANCHI WAENDELEA KUNUFAIKA NA OFA ZA TTCL SABASABA 2026

Maafisa wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wanaendelea kuwahudumia wananchi wanaotembelea Banda la TTCL katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), kwa kuwapatia elimu kuhusu huduma na suluhisho mbalimbali za mawasiliano na teknolojia za kidijitali zinazotolewa na TTCL.

News
July 6, 2026 17:42:31 | By Ester Mbanguka MKURUGENZI MKUU TTCL ATEMBELEA MABANDA YA TAASISI ZA MBALIMBALI SABASABA 2026

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Moremi Marwa, ametembelea mabanda ya taasisi mbalimbali zinazoshiriki Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), kwa lengo la kujionea ubunifu wa teknolojia, kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na kutambua fursa zinazoweza kuchochea maendeleo ya uchumi wa kidijitali nchini.

News
July 4, 2026 19:36:11 | By Ester Mbanguka MKURUGENZI MKUU TTCL AWAKARIBISHA WANANCHI KUJIONEA SULUHISHO ZA KIDIJITALI SABASABA 2026

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Moremi Marwa amewaalika wananchi kutembelea Banda la TTCL katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026) ili kujionea mageuzi ya kiteknolojia na suluhisho mbalimbali za kidijitali zinazotolewa na Shirika katika kuimarisha huduma za mawasiliano na kuchochea uchumi wa kidijitali nchini.

News
July 4, 2026 19:32:05 | By Ester Mbanguka BALOZI WA ANGOLA NCHINI TANZANIA ATEMBELEA BANDA LA TTCL SABASABA 2026

Balozi wa Jamhuri ya Angola nchini Tanzania, Mheshimiwa Domingos Coelho, ametembelea Banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere.