info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

WANANCHI WAENDELEA KUNUFAIKA NA OFA ZA TTCL SABASABA 2026

WANANCHI WAENDELEA KUNUFAIKA NA OFA ZA TTCL SABASABA 2026

Maafisa wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wanaendelea kuwahudumia wananchi wanaotembelea Banda la TTCL katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), kwa kuwapatia elimu kuhusu huduma na suluhisho mbalimbali za mawasiliano na teknolojia za kidijitali zinazotolewa na TTCL.

Katika banda hilo, wananchi wanapata fursa ya kujionea huduma za intaneti ya kasi ya juu, suluhisho za kidijitali kwa matumizi ya nyumbani na biashara, pamoja na kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na TTCL.

Sambamba na hilo, TTCL inaendelea kuwapatia wateja ofa maalum za Sabasaba, zikiwemo vifaa vya mawasiliano vinavyopatikana kwa bei zenye punguzo kubwa, pamoja na huduma mbalimbali zinazolenga kurahisisha maisha na shughuli za kila siku katika mazingira ya kidijitali.

Aidha,wananchi na wadau wanaotembelea banda hilo wanapata fursa ya kutumia buree public Wi-Fi inayopatikana katika viwanja hivyo ili kufahamu speed ya intanet ya TTCL.

TTCL inaendelea kuwakaribisha wananchi wote kutembelea Banda la Shirika hilo katika Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere ili kujionea teknolojia bunifu, kupata elimu kuhusu huduma za mawasiliano na kunufaika na ofa maalum zinazopatikana katika kipindi chote cha maonesho.