info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

TTCL INAENDELEA KUTOA HUDUMA NA ELIMU KWA WAKULIMA NA WANANCHI NANENANE 2026

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) linaendelea kutoa huduma na elimu kwa wakulima na wananchi wanaotembelea Maonesho ya Nanenane 2026 yanayofanyika katika Uwanja wa John Malecela Nzuguni, jijini Dodoma.

Kupitia Banda la Serikali Na. 2, TTCL inawapatia wananchi fursa ya kujifunza na kupata huduma mbalimbali za mawasiliano na TEHAMA, ikiwemo Faiba Mlangoni Kwako, Utunzaji data kimtandao kupitia kituo cha NIDC huduma za Simu na Data, pamoja na suluhisho mbalimbali za kidijitali.

Huduma na elimu hiyo inalenga kuwawezesha wakulima, wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kutumia teknolojia ya mawasiliano katika kuboresha shughuli zao, kuongeza ufanisi na kufungua fursa mpya za kiuchumi na kidijitali.

TTCL inawakaribisha wananchi wote kutembelea Banda la Serikali Na. 2, kupata elimu, ushauri na huduma mbalimbali za kidijitali zinazorahisisha maisha.

#TTCL #Nanenane2026 #Nanenane #Wakulima #TEHAMA #Mawasiliano #BandaLaSerikali#DigitalTanzania #FaibaMlangoniKwako #PublicWiFi #UniWiFi #Dodoma