info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

TTCL YAJA NA OFA KABAMBE MSIMU WA MAONESHO YA NANE NANE 2026

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limetangaza ofa kabambe ya punguzo la bei kwenye vifaa vya intaneti kwa wananchi wanaotembelea banda lake katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nane Nane 2026, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha matumizi ya teknolojia ya kidijitali na kuongeza upatikanaji wa huduma bora za mawasiliano nchini.

Kupitia ofa hiyo, TTCL inatoa punguzo kubwa kwenye vifaa mbalimbali vya intaneti ikiwemo router, MiFi, dongle, wingle na vifaa vingine vya mawasiliano, hatua inayolenga kuwawezesha wakulima, wafugaji, wavuvi, wajasiriamali na wananchi kwa ujumla kupata huduma za intaneti ya kasi kwa gharama nafuu.

Huduma hizo zinatarajiwa kuwawezesha watumiaji kupata taarifa muhimu kwa wakati, ikiwemo taarifa za masoko, hali ya hewa, huduma za kifedha, elimu na fursa mbalimbali za biashara, hivyo kuongeza tija katika uzalishaji na kuchangia ukuaji wa uchumi wa kidijitali.

Akizungumza katika maonesho hayo, Meneja wa Uhamasishaji wa bidhaa wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bi. Janet Maeda, amewakaribisha wananchi wote kutembelea banda la TTCL (Government Pavilion 2) katika uwanja wa John Samwel Malecela Nzuguni Jijini Dodoma, ili kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo pamoja na kunufaika na punguzo maalumu la vifaa vya intaneti vinavyopatikana kwa kipindi chote cha maonesho.

"Maonesho ya Nane Nane ni fursa muhimu ya kuwafikia wananchi na kuwawezesha kupata huduma za mawasiliano na intaneti kwa gharama nafuu. Tunawakaribisha wakulima, wafugaji, wajasiriamali na wananchi wote kutembelea banda letu ili wapate ushauri, huduma bora na kunufaika na ofa hii ya kipekee," amesema Bi. Maeda.

Mbali na punguzo la vifaa vya intaneti, TTCL pia linaendelea kutoa suluhisho mbalimbali za mawasiliano zinazowawezesha wananchi na taasisi kutumia teknolojia ya kidijitali katika shughuli zao za kila siku, hatua inayochochea ubunifu, kuongeza tija na kufungua fursa zaidi za uchumi wa kidijitali.