info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

ZIARA YA WAJUMBE WA BODI SABA SABA

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni Tanzu ya T-Pesa pamoja na Bodi ya Wadhamini ya T-Pesa wamefanya ziara katika banda la TTCL katika Maonesho ya Kimataifa  ya Biashara (Saba Saba) na kufurahishwa na shirika linavyopiga hatua katika kuhakikisha linaendana na kasi ya Teknolojia katika sekta ya Mawasiliano duniani.

Mbali na Wajumbe hao Banda la TTCL limeendelea kupokea Wageni mbalimbali ambapo Maonesho ya 48 yanaendele katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na kujionea shirika linavyopiga hatua katika uendeshaji wa Miradi ya Serikali ya kimkakati ikiwa ni pamoja na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na Kituo Mahili cha Kutunza Kumbukumbu (Data Centre) ambayo imekuwa chachu katika kuleta matokeo chanya nchini.

Viongozi hao ni pamoja Waziri wa Nchi anayeshughulikia masuala ya Majimbo na Ugatuzi kutoka Zimbabwe Mhe. Ezra Chadzamira, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Emmanuel Tutuba, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Tigo Bw. Jerome Albou pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya T-Pesa Bi. Mwanahiba Mzee.

TTCL inashiriki Maonesho haya kama mdau muhimu wa maendeleo ya Biashara na Viwanda kwakuhakikisha upatikanaji wa huduma ya intaneti ni ya uhakika ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa kazi za kibiasha na uwekezaji nchini.

.