WIZARA NA TAASISI ZAKE YAWASILISHA TAARIFA MBELE YA KAMATI YA MIUNDOMBINU
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na taasisi zake za Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Shirika la Posta Tanzania (TPC) imewasilisha taarifa ya ujenzi wa miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na taarifa ya utekelezaji ya TPC kwa Kamati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu tarehe 21 Oktoba 2024 Bungeni jijini Dodoma.
Katika hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw. Selemani Moshi Kakoso (Mb.) na ujumbe wa Wizara na taasisi hizo uliongozwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb) huku mawasilisho yakitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), CPA Moremi Marwa na Posta Masta Mkuu, Bw. Macrice Mbodo.