WAZIRI SILAA ZIARANI MKOANI SINGIDA
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Jerry Silaa (Mb) ameanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Singida kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.
Akiwa mkoani humo Mhe. Silaa amepokelewa na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Halima Dendegu pamoja na Viongozi mbalimbali wa Chama na serikali.
Akiwa katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Waziri Slaa ameleza dhamira ya serikali ya kuwaletea Wananchi wa Mkoa huo maenendeleo katika sekta ya afya, elimu, maji, kilimo na kuimarisha miundombinu ya mawasiliano, hususan katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa mkoa wa Singida.
Alisema Mawasiliano ni nyenzo muhimu hivyo serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa ya kuwasiliana kutumia teknolojia ya kisasa katika shughuli za kila siku, ikiwemo biashara, elimu, na huduma za afya.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa Mhe. Halima Dendego alipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha hali ya maisha ya Wananchi wa Mkoa huo kwani umeendelea kupata manufaa makubwa kutokana na miradi mbalimbali ya serikali inayolenga kuboresha huduma ya mawasiliano, maji, elimu, afya na miundombinu ya Barabara.