info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

WANAWAKE TTCL ZIARANI NGORONGORO

Machi 7 mwaka huu Wanawake wa TTCL waliungana na Wanawake wenzao Zaidi ya 400 kutoka Taasisi, mashirika, Kampuni na Sekta binafsi kufanya ziara maalum katika Hifadhi ya Ngorongoro ili kujionea uzuri wa urithi wa asili wa Tanzania. 

Ziara hii ilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya Kimataifa ya Wanawake duniani kote ikiwa na lengo la kuwapa fursa ya kujifunza kuhusu uhifadhi wa mazingira na namna sekta ya teknolojia inavyoweza kusaidia katika kulinda maliasili za Taifa. 

Wakiwa hifadhini, walishuhudia wanyamapori mbalimbali kama vile Simba, Tembo, na Faru, Pundamilia, Swala na ndege mbalimbali huku wakijifunza kuhusu jitihada za kuhifadhi viumbe hao adimu.

Katika ziara hii Wanawake wa TTCL waliendelea kushirikiana na wanawake kutoka taasisi mbalimbali katika suala la utalii ili kuhakikisha kuwa wanawake wanapata nafasi zaidi katika sekta hii muhimu kwa maendeleo ya taifa.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Kimataifa, 2025 yalifanyika jijini Arusha ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yakibebwa na kauli mbiu "Wanawake na Wasichana 2025, Tuimarushe Haki, Usawa na Uwezeshaji"

.