
WANAFUNZI WA SHREE HINDU MANDAL WAFANYA ZIARA TTCL
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Shree Hindu Mandal wamefanya ziara ya mafunzo katika Makao makuu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) yaliyopo Posta jijini Dar es Salaam.
Ziara hiyo ililenga kuwapatia wanafunzi uelewa wa vitendo kuhusu sekta ya mawasiliano nchini, huku wakipata nafasi ya kujifunza historia ya TTCL na huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika, ikiwemo huduma za intaneti ya kasi, mawasiliano ya simu na mifumo ya kisasa ya kidigitali.
Aidha, Wanafunzi walipata elimu juu ya mifumo ya utunzaji na usalama wa data, ambapo walishuhudia namna TTCL inavyowezesha mawasiliano salama na ya uhakika kwa wateja wake nchini kote.
TTCL itaendelea kushirikiana na shule na jamii kwa ujumla katika kutoa elimu na kuwajengea vijana uelewa wa teknolojia za mawasiliano, ili kuandaa kizazi cha kesho chenye maarifa ya kidigitali.