info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

WAFANYAKAZI WA BUNGE LA MAREKANI WAFANYA ZIARA TTCL

Wafanyakazi wa Bunge la Marekani (Congressional Staff) Oktoba 17, 2024 walifanya ziara katika Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani katika sekta ya mawasiliano na teknolojia ya kidigitali. 

Wafanyakazi hao walipokelewa na Mwenyeji wao ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, CPA Moremi Marwa, pamoja na Maafisa wa shirika hilo, ambapo pamoja na mambo mengine walijadili muhimu wa kuendeleza sekta ya mawasiliano ambayo ni kiini cha maendeleo endelevu ya ujenzi wa Tanzania ya uchumi wa kidigitali. 

Aidha ziara hii ni mwendelezo wa mafanikio ya ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, hapa nchini mwezi Machi 2023 kufuatia mwaliko wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaliko ambao ulilenga kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili, hasa kwenye sekta za teknolojia na uchumi wa kidigitali.

Ziara hii ni hatua muhimu katika kuhakikisha Tanzania inaendelea kufaidika na mapinduzi ya teknolojia ya kidigitali, ambayo ni nyenzo muhimu kwa ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kijamii.