VIONGOZI WA TTCL WATEMBELEA BANDA LA TTCL SABASABA 2026, WASISITIZA HUDUMA BORA KWA WATEJA
Baadhi ya Viongozi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wametembelea banda la TTCL katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Wakati wa ziara hiyo, viongozi hao walipata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na TTCL pamoja na ofa maalum zinazotolewa kwa wateja katika kipindi cha Maonesho ya Sabasaba 2026.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Mkurugenzi wa Ufundi, Mhandisi Cecil Francis, amewataka watumishi wanaohudumu katika banda hilo kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja, kuwahudumia kwa weledi na kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali za TTCL.
Aidha, amewakaribisha wananchi na wateja wote kutembelea banda la TTCL ili kujionea suluhisho mbalimbali za kidijitali zinazotolewa na TTCL na kunufaika na ofa za Sabasaba 2026, pamoja na kutumia huduma ya TTCL Public Wi-Fi inayopatikana bure ndani ya banda la TTCL.
#Sabasaba2026
#TTCL Supersonic Experience Powering Tanzania's Digital Future
#MaoneshoYaBiashara
#Ishikidigitali