info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

TTCL YATOA MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI KINYAMWEZI

Wanafunzi wa Kidato cha Nne kutoka Shule ya Secondari Kinyamwezi wamefanya ziara ya kujifunza masuala mbalimbali ya teknolojia ya mawasiliano katika Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation.

Katika ziara hiyo wamejifunza kuhusu teknolojia ya mawasiliano, huduma za intaneti, na jinsi teknolojia inavyoendelea kubadilika na hivyo wameweza kupata ufahamu wa fursa za ajira katika sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano. 

Aidha Wanafunzi hao waliweza kupata uelewa kuhusu dhana msingi ya Tehama, pamoja na jinsi mitandao, vifaa vya kompyuta, na programu mbalimbali zinavyoweza hutumika kufanya kazi pamoja na kurahisisha utekelezaji wa kazi.

Walifundishwa pia juu ya matumizi salama ya mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na kuheshimu faragha, kuepuka mienendo hatari mtandaoni na kuzitambua fursa za kazi katika Tehama ikiwa ni pamoja na uhandisi wa programu, wataalamu wa usalama wa mtandao, na ubunifu wa tovuti.

Kupitia mafunzo haya, wanafunzi waliweza kuimarisha ustadi wao na kuelewa jinsi Tehama inavyoboresha maisha yao ya kila siku na fursa za kazi zilizopo.