info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

TTCL YALETA MAPINDUZI YA KIDIJITALI NCHINI – MWAKAGENDA

Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni Mwakilishi wa Wanawake Mkoa wa Mbeya, Sophia Mwakagenda amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania -TTCL kwa kuiunganisha nchi kidigitali.

Aliyasema hayo Jijini Dodoma alipotembelea Banda la Maonesho la Shirika hilo kwenye Maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika katika Viwannja vya Nzuguni na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo katika kuhakikisha mawasilia yanapatikana nchi nzima.

Alisema maboresho makubwa yaliyoyafanywa na TTCL katika kuhudumia Umma wa Watanzania hasa katika ulimwengu wa kidigitali hakuna yeyote anayeweza kutia shaka katika hilo kwani shirika hilo linatoa huduma ya intaneti ya kisasa zaidi ya faiba mpaka majumbani bure ili kuwawezesha wananchi kufanya shughuli zao kidigitali na hivyo kuharakisha maendeleo nchini.

 “Niipongeze sana Serikali chini ya usimamizi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia shirika hili la TTCL kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika tumeona sasa mtandao wa interneti unapatikana kila sehemu na ukizingatia sasa hivi Dunia ipo kiganjani”, Alisema.

Aidha alisema kuwa maboresho yaliyoafanyika wao kama jicho la pili la serikali wameridhishwa na kuahidi kushirikiana na serikali kuhakikisha mtandao wa TTCL unafika mbali zaidi.

Aliongeza kuwa sekta ya biashara kwa sasa inategemea zaidi mtandao imara na makini ili kuzifanya biashara hizo kuwafikia walegwa kwa wakati na usalama zaidi hivyo kuimarika kwa shirika hilo kunatoa fursa kwa Wanyabishara kufanya biashara zao kimtandao na kupelekea uchumi wa nchi kuwa imara Zaidi.

Katika hatua nyingine Mhe. Mwakagende alisema kuanza kwa kwa huduma ya safari ya Treni ya Umeme (SGR) kunategemea zaidi uwepo na uimara wa mtandao wa intaneti katika ukataji wa tiketi ili kuondokana na mfumo wa zamani wa ukataji tiketi madirishani na hivyo kuwepo kwa msungamano wa watu na usumbufu usiyo wa lazima hivyo anaamini TTCL atakuwa mtoa huduma ya intaneti wa TRC ili kuiwezesha mifumo ikiwemo ya ukataji tiketi kufanya kazi kwa ufanisi.

Mbali na pongezi hizo Mhe. Mwakagenda alitoa rai kwa shirika hilo kuhakikisha wanafikisha huduma ya intaneti katika shule za Sekondari nchini zilizopo vjijini ili kuzisaidia shule hizo walimu kufundisha na wanafunzi kujifunza kwa vitendo.

“Niwaombe TTCL kupeleka huduma hii kwa shule za Sekondari zilizopo vijijini wapate huduma hii kwenye maktaba zao na maabara zao ili waweze kujifunza kwa vitendo”,Alisema Mwakagenda.