TTCL YAENDELEA KUHAMASISHA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA ELIMU YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA
Na Godfrey Andafiche
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeshiriki mkutano wa Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam uliofanyika tarehe 13 Novemba 2026 katika Ukumbi wa CRDB Makao Makuu, jijini Dar es Salaam, kujadili nafasi ya teknolojia katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Akizungumza katika mkutano huo, Meneja Mauzo na Usambazaji wa TTCL, Bw. Leonard Laibu, ameeleza namna huduma na suluhisho za kiteknolojia zinazotolewa na TTCL zinavyowezesha upatikanaji wa mawasiliano ya uhakika, kurahisisha usambazaji wa taarifa na kuongeza fursa za matumizi ya teknolojia katika kuelimisha jamii.
Huduma hizo ni pamoja na intaneti ya kasi ya FTTH, huduma za simu za mkononi, Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB), Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data Kimtandao (NIDC), Collocation na Kituo cha Huduma kwa Wateja (Call Centre).
Kupitia ushiriki huo, TTCL imesisitiza dhamira yake ya kushirikiana na wadau wa habari kutumia teknolojia kuelimisha jamii, kusambaza taarifa sahihi na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa maendeleo endelevu ya Taifa.
#TTCL #TeknolojiaKwaMaendeleo #NishatiSafiYaKupikia #DigitalTransformation #Tanzania