info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

TTCL QUEENS MABINGWA WAAJIRI HEALTH BONANZA 2023

Timu ya TTCL ya Mpira wa Pete (TTCL Queens) imeibuka kidedea katika Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kuzishirikisha Taasisi, Mashirika na Kampuni mbalimbali nchini.

Bonanza hilo limefanyika leo Octoba 7, 2023 katika Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam huku mgeni Rasmi akiwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Prof. Joyce Ndalichako 

TTCL Queens ilifanikiwa kufuzu hatua zote na kufanikiwa kutinga fainali ambayo iliwakutanisha na timu ya NSSF na hivyo kuwalazimisha wapinzani hao kuondoka na magoli 11 dhidi ya 26  iliyojishindia TTCL Queens.

Ushindi huo umeifanya TTCL Queens kufika Meza Kuu kuvalishwa midali pamoja na kupokea Kombe la Ubingwa kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Prof. Joyce Ndalichako.

#michezokwaafyayaakili

.