info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

TTCL NGUZO YA MAWASILIANO YA KASI KATIKA KUJENGA NA KUIMARISHA SEKTA YA USAFIRISHAJI NCHINI

Na Spencer Julius

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kudhihirisha nafasi yake ya kimkakati katika kuijenga Tanzania ya kidijitali kwa kuwezesha upatikanaji wa huduma za intaneti ya kasi na mawasiliano ya uhakika katika Wiki ya Maadhimisho ya Pili ya Usafirishaji Endelevu Ardhini 2026, iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA).

Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, kuanzia Novemba 24 hadi 26, 2026, yamehitimishwa leo huku TTCL ikiwa miongoni mwa wadau muhimu wanaochangia kuimarisha matumizi ya teknolojia katika shughuli za kijamii na kiuchumi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Mtaalamu wa Biashara kutoka TTCL, Bw. Hilal Mwinyi, amesema TTCL inaendelea kutekeleza dhamira yake ya kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kidijitali kwa kuhakikisha sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya usafirishaji zinapata huduma za mawasiliano ya kasi, salama na ya uhakika.

Ameeleza kuwa mawasiliano ya intaneti ya kasi ni nyenzo muhimu katika mageuzi ya sekta ya usafirishaji, kwani yanawezesha mifumo ya kidijitali kufanya kazi kwa ufanisi, kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa wakati na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Kupitia uwekezaji katika miundombinu ya kisasa ya mawasiliano, ikiwemo Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na huduma za intaneti ya kasi, TTCL inaendelea kuwa kiungo muhimu kati ya teknolojia, taasisi na wananchi, ikiwezesha sekta mbalimbali kutumia fursa za kidijitali katika kuongeza tija na ufanisi.