TTCL MUHIMILI WA MAWASILIANO NCHINI, DC LONGIDO APONGEZA HUDUMA ZA SHIRIKA
Na Spencer Julius
Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe. Salum Abdalah Kalli, amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa mchango wake katika kuimarisha sekta ya mawasiliano nchini na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na za uhakika, ikiwemo huduma ya intaneti kupitia Faiba Mlangoni Kwako.
Mhe. Kalli ametoa pongezi hizo alipotembelea Ofisi za TTCL Mkoa wa Arusha, ambapo alipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Shirika katika kuboresha huduma na kuwafikia wateja.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Kalli amesema TTCL inaendelea kuwa muhimili muhimu wa mawasiliano nchini, kutokana na nafasi yake katika kuwezesha upatikanaji wa huduma za mawasiliano zinazochangia shughuli za kijamii, kiuchumi na kiusalama.
“TTCL imekuwa muhimili wa mawasiliano nchini. Kupitia huduma zake za uhakika, tumeona jinsi usalama wa nchi unavyoimarika na wananchi wanavyofaidika na mawasiliano bora, ikiwemo huduma ya intaneti ambayo sasa inapatikana kwa uhakika zaidi majumbani na maeneo mengine,” amesema Mhe. Kalli.
Aidha, amepongeza jitihada za TTCL za kusogeza huduma za intaneti karibu zaidi na wananchi kupitia Faiba Mlangoni Kwako, akibainisha umuhimu wa huduma za mawasiliano ya uhakika katika maisha ya kila siku na maendeleo ya jamii.
Kwa upande wake, Meneja wa TTCL Mkoa wa Arusha, Mhand. Amani Kichele, amemhakikishia Mkuu huyo wa Wilaya kuwa TTCL itaendelea kuimarisha miundombinu na kuboresha huduma zake ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya mawasiliano na huduma za kidijitali.
Mhand. Kichele amesema kupitia Faiba Mlangoni Kwako, TTCL inalenga kurahisisha upatikanaji wa intaneti ya kasi na ya uhakika kwa kuifikisha huduma moja kwa moja katika makazi ya wananchi.
“Tunaendelea kuwekeza katika miundombinu ili kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora za mawasiliano. Faiba Mlangoni Kwako ni sehemu ya dhamira yetu ya kusogeza huduma ya intaneti ya uhakika karibu zaidi na wananchi,” amesema Mhand. Kichele.
TTCL inaendelea na dhamira yake ya kujenga Tanzania iliyounganishwa kidijitali kwa kutoa huduma za mawasiliano zenye ubora, uhakika na zinazokidhi mahitaji ya wa