info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

T-PESA WADHAMINI NGAO YA JAMII 2026 ZANZIBAR

Na Emerco Mashelle

Kampuni Tanzu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), T-PESA, kupitia huduma yake ya N-card, imeendelea kudhihirisha dhamira yake ya kuunga mkono maendeleo ya soka Zanzibar kwa kudhamini na kushiriki kikamilifu katika Mchezo wa Ngao ya Jamii 2026 uliozikutanisha KVZ FC na KMKM SC uliofanyika tarehe 23 Agosti 2026 katika Uwanja wa Mao, Zanzibar.

Katika kuhakikisha mashabiki wanapata uzoefu bora, T-PESA ilishiriki kupitia huduma yake ya N-card, iliyowezesha ununuzi wa viingilio kwa urahisi na kuchangia kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha katika uwanja wa michezo. Ushiriki huo umeendelea kuonesha namna teknolojia ya kifedha inavyoweza kuunganishwa na michezo kwa manufaa ya mashabiki na waandaaji.

Uwepo wa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mhe. Dkt. Riziki Pembe Juma, pamoja na viongozi mbalimbali wa michezo, uliweka uzito zaidi katika tukio hilo na kuonesha umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta ya michezo na wadau wa sekta binafsi katika kukuza vipaji na mashindano ya ndani.

Kumalizika kwa Ngao ya Jamii 2026 kwa mafanikio kunaashiria mwanzo wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Soka Zanzibar, huku T-PESA ikiendelea kuwa sehemu ya safari hiyo kupitia udhamini wake na huduma za kisasa za kifedha. Udhamini huu unaendelea kuthibitisha dhamira ya T-PESA ya kutumia michezo kama nyenzo ya kuunganisha jamii, kukuza vipaji na kuchangia maendeleo endelevu ya soka Zanzibar.