info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

T-FIBER TRIPLE HUB: UVUMBUZI MPYA WA TTCL KWA MAISHA YA KIDIJITALI

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limezindua rasmi kifurushi kipya cha Faiba Mlangoni Kwako kinachoitwa T-Fiber Triple Hub, kifurushi cha kipekee kinachounganisha huduma tatu muhimu: Intaneti ya kasi isiyo na kikomo, huduma ya simu ya mezani (Voice Service), na huduma ya intaneti pamoja na dakika kwa simu ya mkononi. Uzinduzi huo umefanyika leo katika makao makuu ya shirika la Mawasiliano Tanzania jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Meneja wa Masoko wa TTCL, Bi. Janeth Maeda, ameeleza kuwa dunia ya sasa inaendeshwa na teknolojia, hivyo TTCL imewekeza kwa nguvu kuhakikisha Watanzania wanapata huduma za mawasiliano zenye kasi, ubora na gharama nafuu. “Kupitia T-Fiber Triple Hub, tunalenga kurahisisha maisha ya Watanzania kwa kuwapa huduma zote muhimu kwa kifurushi kimoja na bili moja,”. Huduma hii inalenga familia, biashara ndogo na kubwa, pamoja na taasisi zinazohitaji mawasiliano ya uhakika na yenye thamani halisi.

Kwa gharama nafuu kuanzia shilingi 70,000 kwa mwezi, wateja wa T-Fiber Triple Hub wanapata intaneti ya kasi hadi 20 Mbps (upload na download), dakika 300 za mawasiliano ya mezani, pamoja na GB 20 kwa matumizi ya simu ya mkononi. Kifurushi hiki kinatoa urahisi wa kipekee kwani mteja anaweza kufurahia huduma tatu kwa pamoja popote alipo, kupitia miundombinu imara ya TTCL.

TTCL imeeleza kuwa uzinduzi wa T-Fiber Triple Hub ni ishara ya mageuzi mapya katika mawasiliano ya kidijitali nchini Tanzania. Huduma hii ni sehemu ya juhudi za shirika kuunga mkono ajenda ya serikali ya kuongeza matumizi ya TEHAMA na kuunganisha Watanzania wote katika mfumo wa kidijitali. “Tunawaalika Watanzania wote kujiunga nasi katika hatua hii mpya ya ubora, urahisi, na thamani kupitia T-Fiber Triple Hub,” alihitimisha Bi. Maeda.T-Fiber Triple Hub, kifurushi cha kipekee kinachounganisha huduma tatu muhimu: Intaneti ya kasi isiyo na kikomo, huduma ya simu ya mezani (Voice Service), na huduma ya intaneti pamoja na dakika kwa simu ya mkononi. Uzinduzi huo umefanyika leo katika makao makuu ya shirika la Mawasiliano Tanzania jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Meneja wa Masoko wa TTCL, Bi. Janeth Maeda, ameeleza kuwa dunia ya sasa inaendeshwa na teknolojia, hivyo TTCL imewekeza kwa nguvu kuhakikisha Watanzania wanapata huduma za mawasiliano zenye kasi, ubora na gharama nafuu. “Kupitia T-Fiber Triple Hub, tunalenga kurahisisha maisha ya Watanzania kwa kuwapa huduma zote muhimu kwa kifurushi kimoja na bili moja,”. Huduma hii inalenga familia, biashara ndogo na kubwa, pamoja na taasisi zinazohitaji mawasiliano ya uhakika na yenye thamani halisi.

Kwa gharama nafuu kuanzia shilingi 70,000 kwa mwezi, wateja wa T-Fiber Triple Hub wanapata intaneti ya kasi hadi 20 Mbps (upload na download), dakika 300 za mawasiliano ya mezani, pamoja na GB 20 kwa matumizi ya simu ya mkononi. Kifurushi hiki kinatoa urahisi wa kipekee kwani mteja anaweza kufurahia huduma tatu kwa pamoja popote alipo, kupitia miundombinu imara ya TTCL.

TTCL imeeleza kuwa uzinduzi wa T-Fiber Triple Hub ni ishara ya mageuzi mapya katika mawasiliano ya kidijitali nchini Tanzania. Huduma hii ni sehemu ya juhudi za shirika kuunga mkono ajenda ya serikali ya kuongeza matumizi ya TEHAMA na kuunganisha Watanzania wote katika mfumo wa kidijitali. “Tunawaalika Watanzania wote kujiunga nasi katika hatua hii mpya ya ubora, urahisi, na thamani kupitia T-Fiber Triple Hub,” alihitimisha Bi. Maeda.