RAIS DKT. MWINYI ATEMBELEA BANDA LA TTCL SABA SABA 2024
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi ametembelea Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba) na kupokelewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Cecil Francis.
Akiwa katika Banda hilo Rais Dk. Mwinyi alioneshwa huduma zinazotolewa na TTCL pamoja na mchango wa Shirika hilo katika Sekta ya Mawasiliano hapa nchini.
TTCL imetumia fursa hiyo pia kumuonesha Dk. Mwinyi maendeleo yaliyofikiwa katika utekelezaji wa majukumu ya Shirika kwa Wananchi ya kuhakikisha huduma za Mawasiliano inawakia kikamilifu.
Katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba kwa mwaka 2024 ambayo yamehitimishwa leo Julai 13, TTCL imeshika nafasi ya pili na kupata tuzo katika kipengele cha Sekta ya Mawasiliano nchini.
Maonesho hayo yamefungwa rasmi na Mheshimiwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi.
Maonesho ya Saba Saba yanayofanyika kila mwaka hapa nchini. Mwaka huu yanabebwa na Kauli mbiu “Tanzania ni Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji” ambapo TTCL ilibeba kauli mbi hii kama fursa muhimu ya kujinasibu kiteknolojia na kuonesha inavyochangia katika kukuza biashara na kuongeza mvuto wa Wawekazaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza nchini.
Katika maonesho haya TTCL imeonesha jinsi ilivyoungezea thamani Mlima Kilimanjaro kwakuuwekea miundombinu ya mawasiliano ya intaneti na hivyo kuufanya mlima huo kuwa na kivutio cha kipekee na kupeleka watalii kuongezeka.
Banda la TTCL lilijikita katika kuonesha nguvu ya huduma inayotolewa katika mlima Kilimanjaro kutokana na intanet yenye kasi zaidi ambapo wananchi wamekuwa wakipanda mlima huo live kwanjia ya video moja kwa moja kutoka Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Aidha shirika lilijikta katika kuwapa elimu wananchi waliofika katika banda la maonesho juu ya maana na umuhimu wa uwepo wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kuwajengea uelewa jinsi mkongo unavyoleta mapinduzi makubwa katika matumizi ya TEHAMA nchini.