info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

NITAZIONDOA CHANGAMOTO NDANI YA TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA – RAIS DKT SAMIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan aahidi kuondoa changamoto zinazozikabili Taasisi na Mashirika ya Umma ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Rais ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha Siku Tatu cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma nchini kinachofanyika jijini Arusha. tarehe 19-21 Agosti, 2023.Kikao hiko ni mwendelezo wa vikao ambavyo vimekuwa vikifanyika katika ngazi mbalimbali Serikalini kwa lengo la kuboresha utendaji ili mashirika ya Umma yafanye kazi kwa ufanisi na wenye tija.

Mhe. Rais amesema, Serikali imeanza kurekebisha masuala mbalimbali katika sheria na taratibu za ununuzi wa umma ili Mashirika yakazalishe.Amesema Serikali imetoa uhuru kwa Taasisi kujiendesha katika mambo ya msingi, kufanya maboresho ya ajira kwa watumishi wao.Aidha Serikali imepanga kuanzisha Mfuko wa Uwekezaji wa Umma ili kuondoa utegemezi kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali.

Pamoja na hayo yote, Mhe. Rais ametoa rai kwa Viongozi hao kufanya kazi kwa bidii na kutekeleza majukumu yao ipasavyo ili kujenga uchumi wa Tanzania.

Mwenyekiti wa Bodi Bi. Zuhura S.Muro na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania -TTCL  Mhandisi Peter R. Ulanga washiriki Kikao hicho.

 

.