info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

NAIBU WAZIRI DKT. MKAMA AWASILISHA TAARIFA YA UTENDAJI WA NIDC KAMATI YA BAJETI

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Switbert Zacharia Mkama (Mb), amewasilisha taarifa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika kikao kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma tarehe 13 Mei 2026.

Kikao hicho kiliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Ally Hassan Omar King (Mb), ambapo wajumbe walipata fursa ya kujadili na kutoa ushauri kwa Serikali kuhusu Taarifa ya Utendaji wa Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Data Kimtandao (NIDC).

Akizungumza baada ya michango mbalimbali ya wajumbe wa kamati hiyo, Naibu Waziri Dkt. Mkama aliishukuru Kamati kwa michango na ushauri walioutoa, huku akibainisha kuwa Serikali itaendelea kuufanyia kazi ushauri huo ili kuimarisha utendaji na maendeleo ya sekta Mawasiliano na Teknolojia ya Habari nchini.
Katika kikao hicho, TTCL iliwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu Moremi Marwa pamoja na viongozi waandamizi wa Shirika.