info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

MAKAMU WA RAIS, DKT. MPANGO AZIAGIZA TAASISI NA MASHIRIKA MIFUMO KUSOMANA

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) linashiriki Kikao Kazi cha Tano cha Serikali Mtandao kinacholenga kuimarisha matumizi ya (TEHAMA) katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Kikao hicki kilichoandaliwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao kimefunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, Februari 11 mwaka huu.

Dkt. Mpango amezipongeza Taasisi na Mashirika ya Umma kwakushirikiana na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e GA) katika kuhakikisha mifumo inayotumiwa na taasisi hizo inasomana na kubadilishana taarifa. 

Aidha amewataka Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma kuhakikisha wanazingatia sheria na kanuni na miongo zilizowekwa na Mamlaka ya serikali Mtandao katika uanzishaji, ujenzi na usimamizi Miradi ya TEHAMA. 

TTCL pamoja na mambo mengine ni mdau muhimu katika Kikao Kazi hiki kutokana na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya TEHAMA kupitia usimamizi na uendeshaji mzuri wa miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB).

Usimamizi huu unalifanya shirika hilo kuwa mtoa huduma mkuu wa mawasiliano kwa taasisi, Mashirika, wizara za serikali, na hivyo kusaidia kufikia hadhima ya serikali ya kuongeza ufanisi na kupunguza gharama katika kurahisisha utoaji na upatikanaji wa huduma kwa wananchi kidigitali.

Aidha kupitia kikao kazi hiki TTCL inapata fursa ya kushirikiana na Taasisi za serikali, sekta binafsi, na wadau wa TEHAMA kujadili, kupanga na kuweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na uhalifu wa kimtandao na kuimarisha ulinzi wa mifumo ya serikali mtandao.

Kikao kazi hiki kimefanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa ICC jijini Arusha na kumewakutanisha Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma, Mashirika binafsi, na Wadau mbalilbali wa TEHAMA.

.