KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAIPONGEZA TTCL KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA KIMKAKATI YA MAWASILIANO
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeipongeza TTCL kwa juhudi zake katika kuimarisha miundombinu ya mawasiliano nchini, pongezi hizo zimetolewa Leo wakati ziara ya kamati hiyo ilifanywa katika Shirika la Mawasiliano Tanzania - TTCL jijini Dar es Salaam.
Ziara hiyo imeongozwa na Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Selemani Kakoso (Mb) imepokelewa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Kairuki pamoja na Menejimenti ya TTCL.
Wajumbe wa Kamati walipata fursa ya kutembelea Kituo cha Usimamizi wa Mtandao (NOC) na Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data (NIDC), ambapo walijionea namna mifumo ya kisasa ya mawasiliano inavyofanya kazi. Huku Mwenyekiti wa Kamati hiyo akilipongeza shirika kwa ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake.
Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, CPA Moremi Marwa, aliwasilisha taarifa ya miradi mbalimbali inayoendelea, huku Serikali ikiendelea kusisitiza uwekezaji katika TEHAMA. TTCL inaendelea kuwa mhimili muhimu katika utoaji wa huduma za mawasiliano na uhifadhi wa data nchini.