info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

VIONGOZI TTCL WASHIRIKI UZINDUZI WA MICHUANO YA AFL

Tanzania imekuwa Mwenyeji wa Uzinduzi wa Michuano Mipya ya African Football League (AFL) iliyoshuhudiwa na viongozi wa soka Barani Afrika na watu maarufu duniani na kuwakutanisha miamba wawili yaani Simba SC ya Tanzania na Al Alhly ya nchini Misri.

Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania –TTCL, Viongozi waandamizi na Wawakili wa Viongozi wa Shirika walikuwa ni miongoni walioungana na Watanzania kushuhudia sherehe hizo kubwa kuwahi kutokea hapa nchini.

Uzinduzi huo ulifuatiwa na mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa michuano hiyo kati ya Wawakilishi kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Simba SC dhidi ya wenzao kutoka Afrika ya Kaskazini na kutanguliwa na burudani mbalimbali.

.