info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

TUTAENDELEA KUIMARISHA MAWASILIANO MKOANI MWANZA ILI KUONGEZA UFANISI: MHA. ULANGA

Mkurugenzi Mkuu Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Mhandisi. Peter Ulanga, ameahidi kuwa shirika hilo litaendelea kuimarisha miundombinu ya mawasiliano mkoani Mwanza ili kuongeza kasi ya maendeleo katika mkoa huo.

Mhandisi Ulanga alitoa ahadi hiyo hivi karibuni alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na kufanya Kikao na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Mohamrd Mtanda ambapo pamoja na mambo mengine kikao hicho kililenga kukuza ushirikiano katika na mahusiano katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za serikali.

Aidha kikao kililenga kuimarisha sekta ya Mawasiliano, utekelezaji katika kuboresha Miundo Mbinu ya Mawasiliano pamoja na kushirikiana katika kufanya mapitio ya miradi ya mawasiliano inayotekelezwa mkoani humo.

Mhandisi Ulanga alisema kuwa Mwanza ni Mkoa muhimu kwa uchumi wa Tanzania hivy shirika hilo lina dhamira ya kuhakikisha unakuwa na miundombinu bora ya mawasiliano itakayowezesha wananchi na wajasiriamali kufikia fursa mbalimbali za kiuchumi kwa njia ya kidigitali.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mohamed Mtanda, aliwapongeza TTCL kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuboresha huduma za mawasiliano nchini na kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa Wananchi. 

Alisema serikali kupitia Mkoa wa Mwanza itaendelea kushirikiana na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na TTCL ili kuhakikisha kuwa wananchi wa Mwanza wanapata huduma bora za mawasiliano na kuzitumia fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye mifumo ya mawasiliano.

Katika ziara hiyo iliyofanyika Aprili 5, Mwaka huu Mkurugenzi Mkuu  aliambatana na Meneja Mratibu wa Mikoa ya Kibiashara ya TTCL Mhandisi. Innocent Msasi na Meneja wa Mkoa wa Mwanza Bw. Semkopwa Jalili.