info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

TTCL YATOA SHUKRANI KWA WASHIRIKI WA KIKAO KAZI CHA WENYEVITI WA BODI NA WAKUU WA TAASISI

Shirika la Mawasiliano Tanzania -TTCL  linatoa shukrani kwa washiriki wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi waliotembelea banda lao la maonesho katika viwanja vya Ukumbi wa AICC Arusha.

Katika tukio hili, TTCL ilipata fursa ya kuwaonyesha washiriki bidhaa na huduma zao mbalimbali, ikiwa ni pamoja na teknolojia mpya za mawasiliano, huduma za simu, data, na huduma za kifedha kama T-PESA.

Maonesho hayo yaliwapa washiriki nafasi ya kujifunza zaidi kuhusu jinsi TTCL inavyoboresha mawasiliano na huduma kwa Watanzania kupitia huduma yao mpya ya Faiba Mlangoni kwako ikiwezeshwa na uwepo wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano NICTBB.

Katika kipindi chote cha maonesho TTCL ilionesha umuhimu wa  ushirikiano wao na taasisi mbalimbali katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za mawasiliano ya data na sauti jinsi unavyo boresha utekelezaji wa majukumu ya Taasisi na Mashirika hayo katika kuwahudumia Wananchi.

Aidha shirika lilionesha jinsi lilivyo na jitihada za kuboresha huduma ili kukidhi mahitaji ya wateja na kuendana na maendeleo ya kiteknolojia.

Kikao Kazi cha Pili cha Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma cha siku nne kilianza Agosti 27 hadi 30 mwaka huu jijini Arusha, kiliandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kikiwa na madhumuni ya kujadili, kupanga, kubadilishana uzoefu na kupokea maelekezo ya Serikali juu ya namna bora ya kuhakikisha mashirika na taasisi wanazozisimamia zinakuwa na tija kwa manufaa ya Wananchi wote.

.