TTCL YATEMBELEA WATEJA SABA SABA
Shirika la Mawasiliano Tanzania -TTCL likiwa ni miongoni mwa Taasisi Mashirika Wajasiriamali na Wafanyabiasha wanaoshiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara alimaarufu Saba Saba Saba 2024 limepata fursa ya kukutana na Wateja na kupata mrejesho kuhusu huduma na bidhaa zinazotolewa na Shirika hilo.
Bi Amina Njechele ni Meneja Mkoa wa Biashara wa Dar es Salaam Kusini June 30 Mwaka huu alitembelea mabanda kadhaa lengo likiwa ni kupata mrejesho wa mwenendo wa huduma inayotolewa na TTCL kwa wateja wa mabanda hayo.
Akiwa katika mabanda hayo aliwaahukuru kwakuendelea kuwa wateja muhimu wa TTCL huku akiwahakikishia kuwa Shirika litaendelea kutoa intaneti inayokidhi mahitaji ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yako katika ubora na kiwango cha juu.
Mabanda yaliyotembelewa na Bi Amina ni pamoja na Benki Kuu ya Tanzania -BOT, Chuo cha Ufundi Stadi VETA pamoja na Shirika la Posta Tanzania.
Tusa Mwakarobo ni Afisa TEHAMA wa Benki Kuu ya Tanzania ameshukuru TTCL kwakufika katika Banda lao huku akisema kitendo hicho ni kizuri kwani kinaonesha jinsi Shirika linavyojali wateja wake.
Kwa upande wake Afisa Habari Mwandamizi wa VETA Bi. Dorah Tesha amesema huduma ya Intaneti inayotolewa na TTCL imekuwa chachu katika kifundishia na kukifanya Chuo hicho kwenda na kasi ya mabadiliko ya Teknolojia nchini.