info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

TTCL YACHANGIA NA KUSHIRIKI CRDB MARATHON 2023

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), limeshiriki  Mbio za CRDB International Marathon Msimu wa Nne ambapo ambapo zililenga kukusanya fedha kwa ajili ya kuwasaidia Wanawake wenye ugonjwa wa Fistula wanaotibiwa katika Hospitali ya CCBRT Jijini Dar es Salaam.

Mbio hizo zilizofanyika Agosti 13, Mwaka huu pia zililenga kuchangia fedha kwa ajili ya Watoto wasiojiweza ambao wamelazwa Hospitali ya Jakaya Kikwete wanasumbuliwa na matatizo ya moyo pamoja na kuchangia ujenzi wa Kituo cha Afya Zanzibar.

TTCL kama mdau ilishiriki mbio hizo zilizojumuisha wanamichezo mbalimbali ikiwemo kutoka Taasisi na Mashirika ya Umma na Watu binafsi lengo likiwa ni kusaidia sekta ya Afya nchini.

Watumishi wa TTCL wameshiriki mbio hizo za kilometa  tano na kilometa kumi.

Mgeni rasmi katika mashindano haya alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mh. Dkt. Hussein Mwinyi ambaye aliongozana na baadhi ya viongozi wa Serikali na Chama akiwemo Waziri wa Michezo wa Tanzania Balozi Dkt. Pindi Chana pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert John Chalamila.