T-PESA YATOA ELIMU KWA WATEJA MAADHIMISHO WIKI YA FEDHA
T- Pesa Kampuni Tanzu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL-Corporation ni miongoni mwa Mashirika na Taasisi za kifedha zilizoshiriki Maadhimisho ya Wiki ya huduma za Fedha Kitafa yaliyoandaliwa na kuratibiwa na Wizara ya Fedha na Mipango lengo likiwa ni kutekeleza mpango wa Maendeleo ya sekta ya fedha wa mwa 2020/ 21-2029/30.
Katika mpango huo elimu kwa umma ni moja ya maeneo ya kipaumbele katika utekelezaji ambapo katika hatua ya utekelezaji Wizara ya Fedha na MIpango iliandaa programu ya kutoa elimu kwa Umma ya mwaka 2021/22-2025/26 na kuweka mikakati mbalimbali itakayotumika katika utoaji wa elimu ya fedha kwa umma.
Moja ya mikakati hiyo ni pamoja na uwepo wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha ya kila mwaka ambapo elimu ya matumizi ya fedha kidigitali inatolewa kwa wananchi.
Tangu kuanza kwa maadhimisho haya ambapo mara ya kwanza yalifanyika jijini Dar es Salaam, mara ya pili yalifanyika jijini Mwanza na mwaka huu 2023 yamefanyika jijini Arusha huku Kampuni ya T-Pesa ikiwa mdau muhimu na mshiriki maadhimisho haya.
Maadhimisho haya yalizishirikisha Taasisi ndogo za fedha, Mabenki, Mifuko ya Hifadhi za Jamii pamoja na wajasiriamali yalisaidia Kampuni ya T-PESA kukutana na Wananchi na kuwajengea uelewa kuhusu matumizi sahihi ya fedha mtandao na fursa mbalimbali zinazopatikana katika Kampuni hiyo zinazoweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.
Aidha maadhimisho hayo pamoja na mambo mengine yalitoa fursa kwa Kampuni hiyo kukutana na Wateja na Wananchi kwa ukubwa zaidi na kujibu hoja, maswali na kero zao na hivyo maadhimisho hayo yamekuwa muhimu katika kupata mrejesho sahihi kuhusu huduma na bidhaa zinazotolewa na T-PESA.
Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yamefanyika kwa mara ya tatu huku kwa mwaka huu huku yakiwa na kaulimbiu, Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi na kuzinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali.