SABA SABA FURSA YA KUKUTANA NA WATEJA NA KUIMARISHA MAHUSIANO KIBIASHARA
Maonesho ya Saba Saba ni maonyesho ya biashara na viwanda yanayofanyika kila mwaka hapa nchini. Mwaka huu yanabebwa na Kauli mbiu “Tanzania ni Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji” ambapo TTCL imebeba kauli mbiu hii kama fursa muhimu ya kujinasibu kiteknolojia na kuonesha inavyochangia katika kukuza biashara na kuongeza mvuto kwa Wawekazaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza nchini.
Mbali na maonesho haya kuwa fursa nzuri kwa TTCL kukutana na wateja wapya na kuimarisha mahusiano na wateja lakini pia ni fursa ya kuhabarisha Umma kuhusu kazi na majukumu shirika lililonalo ya kuimarisha mawasiliano nchini na hasa katika maeneo yote ya kimkakati.
Katika maonesho haya TTCL imeonesha jinsi ilivyouongezea thamani Mlima Kilimanjaro kwakuuwekea miundombinu ya mawasilia ya intaneti na hivyo kuufanya mlima huo kuwa na kivutio cha kipekee na kupeleka watalii kuongezeka.
Banda la TTCL limejikita kuonesha nguvu ya huduma inayotolewa katika mlima Kilimanjaro kutokana na intanet yenye kasi zaidi ambapo wananchi wamekuwa wakipanda mlima huo live kwanjia ya video moja kwa moja kutoka Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam wakahi huu wa maonesho.
Aidha shirika limejikta katika kuwapa elimu wananchi waliofika katika banda la maonesho juu ya maana na umuhimu wa uwepo wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kuwajengea uelewa jinsi mkongo unavyoleta mapinduzi makubwa katika matumizi ya TEHAMA nchini.