info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

MKURUGENZI MKUU TTCL ATEMBELEA MABANDA YA TAASISI MBALIMBALI SABASABA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Moremi Marwa, ametembelea mabanda ya Taasisi mbalimbali za Sekta ya Mawasiliano na Maendeleo ya Viwanda katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya SabaSaba, yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Taasisi alizotembelea ni pamoja na Shirika la Posta Tanzania (TPC), Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), pamoja na Banda la Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Kabla ya kuanza ziara yake, Bw. Marwa alipokelewa rasmi na uongozi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), ambao ndiyo waandaaji wa maonesho hayo, na kupata maelezo kuhusu maandalizi na malengo ya maonesho kwa mwaka huu.

Katika kila banda, alipokelewa na kuelezwa shughuli, huduma na majukumu ya taasisi hizo katika zama hizi za kidigitali.

Ziara hiyo ililenga kuimarisha mahusiano ya kikazi, kuibua fursa mpya za ushirikiano na kuhakikisha malengo ya pamoja ya matumizi ya kidigitali na kiuchumi wa kidigitali yanafikiwa kwa ufanisi na tija kwa maendeleo ya Taifa.