MKURUGENZI MKUU TTCL ASHIRI KIKAO KAZI CHA MSAJILI WA HAZINA -ARUSHA
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, CPA Moremi Marwa ameshiriki Kikao Kazi cha cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi kinachofanyika Arusha katika Ukumbi wa AICC Arusha.
Kikao hiki cha siku Tatu kimezikutanisha Taasisi 248 za Umma na 58 za binafsi kimefunguliwa leo Agosti 28, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Sami Suluhu Hassan.
TTCL ni mdau muhimu katika Kikao kazi hiki ambapo imewezesha huduma ya Intaneti ili kuwarahisishia washiriki kutekeleza shughuli mbalimbali kwa kipindi chote cha Kikao hiki.
Kikao hiki kinalenga kujadili masuala muhimu yanayohusu maendeleo ya sekta mbalimbali, ushirikiano kati ya Taasisi, na mkakati wa kuimarisha utendaji wa Mashirika ya Umma nchini.
Katika hatua nyingine TTCL inatumia fursa ya uwepo wa kikao hiki kuonesha mchango wake katika kuboresha huduma za mawasiliano na teknolojia kupitia Banda la Maonesho lililopo katika Viwanja vya Ukumbi wa AICC Arusha.
Katika banda hilo TTCL inaonesha juhudi za shirika hilo katika kuboresha miundombinu ya mawasiliano na kuleta huduma za kisasa zaidi kwa wananchi.