info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

WAZIRI WA KILIMO ZANZIBAR AIPONGEZA TTCL KWA KUIMARISHA MAWASILIANO.

Waziri wa Kilimo. Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Mhe. Shamata Khamis amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania –TTCL kwa huduma wanazozitoa ambapo zimerahisisha Mawasiliano Nchini Tanzania na nje ya Nchi. Mhe. Shamata ametoa pongezi hizo Agosti 6 mwaka huu alipotembelea banda la TTCL ambapo katika Maonesho ya Madhimisho ya Siku Kuu ya Wakulima (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya. Waziri amepongeza hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na TTCL za kupanua Mawasiliano nchini na ameomba kasi iendelee ili kuweze kutimiza ahadi ya Chama cha Mapinduzi ya kuhakikisha Wananchi wanafikiwa na huduma ya mawasiliano ili kurahisisha huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi. Aidha ametoa wito kwa Wafanyakazi na Viongozi wa shirika hilo kufanya kazi kwa bidii ili kuliwezesha Shirika kusonga mbele katika kutimiza wajibu iliyopewa na serikali wa kuhakikisha linatoa huduma za mawasiliano kwa gharama nafuu. Katika hatua nyingine amelipongeza Shirika hilo kwa kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutangaza sekta ya Utalii kupitia filamu ya Royal Tour ambapo lilifikisha huduma ya Intaneti katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro ili kuwawezesha Watalii kuchukua matukio mbalimbali katika hifadhi hiyo na kuyarusha duniani kupitia mitandao ya kijamii na hivyo kupelea uchumi wa Taifa kukua kupitia sekta hiyo ya Utalii. Amesema kwa sasa anafurahishwa jinsi Shirika hilo linavyoshughulikia malalamiko ya wateja wake na kwamba hii inaonesha ni kiasi gani serikali ya Awamu ya Sita ilivyojidhatiti kuhakikisha shirika hilo linapewa nguvu ya kuwahudumia Wananchi. Kwa upande wake Meneja TTCL Mkoa wa Mbeya Bw. Mujuni Kyaruzi alimshukuru Waziri Shamata kwa kutembelea Banda la TTCL kwani kupitia Maonesho haya elimu ya masuala ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Data center, Public Wi-Fi, Faiba Mlangoni Kwako, T-Pesa na Simu za mkononi yameendelea kutolewa kwa Wananchi na Wadau mbalimbali ili kukuza uelewa kuhusu huduma na bidhaa zinazotolewa na TTCL. Maonesho ya Nanenane mwaka huu 2023 yanayoongozwa na kauli mbiu isemayo “Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula”.