info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

TTCL YADHAMINI MICHUANO YA KIZIMKAZI SAMIA YOUTH CUP 2024

 

Shirika la Mawasiliano Tanzania- TTCL Limedhamini Michuano ya Samia Youth Cup lenye lengo la kukuza vipaji kwa vijana katika michezo hapa nchini.

Katika Michuano hiyo Timu ya Shule ya Sekondari ya Kusini iliibuka Bingwa wa michuano hiyo ya Kizimkazi Samia Youth Cup 2024 baada ya kuichapa Timu ya Shule ya Sekondari Muyuni mabao 3 kwa 0 katika Fainali zilizochezwa Agosti 24, 2024 katika Uwanja wa New Amani Mjini Zanzibar.

Mgeni Rasmi katika fainali hizo alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.  Philip Mpango ambaye pamoja na mambo mengine aligawa zawadi za Hundi, Medali na Kombe kwa Mshindi wa Kwanza hadi wa Tatu.

Mshindi wa kwanza alipata Kombe, Medali na Hundi ya shilingi milioni moja na laki tano, Mshindi wa pili ambaye ni timu ya Shule ya Sekondari Muyuni alipata Medali na Hundi ya shilingi milioni moja taslimu, na Mshindi wa Tatu ni Timu ya Shule ya Sekondari Hasnuu Makame ikipata medali na hundi ya shilingi laki Saba.

Kwa kudhamini michuano hii, TTCL imeonyesha dhamira yake ya kuwekeza katika maendeleo ya vijana kupitia michezo ambapo TTCL katika michuano hiyo ilitoa udhamini wa kifedha na vifaa vya michezo.

Kwa kushirikiana na na Benki ya Biashara ya Taifa (NBC), TTCL iliweka msisitizo kwenye kutumia michuano hiyo kama jukwaa la kuwaibua wachezaji chipukizi ambao wanaweza kuendelezwa zaidi na kuwa nyota wa baadaye katika michezo ya kitaifa na kimataifa.

Ushiriki wa TTCL katika kudhamini Samia Youth Cup 2024 unalenga si tu kuboresha michezo, bali pia kuleta fursa za maendeleo kwa vijana, huku ikihamasisha ushirikiano baina ya jamii na sekta ya mawasiliano katika kujenga Taifa lenye afya na lenye vipaji endelevu kwa vijana.