info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

T-PESA NA NIC ZASHIRIKIANA UTOAJI BIMA KWA WAKUU WA TAASISI

Kampuni Tanzu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania, T-PESA Limited na Shirika la Bima (National Insurance Corporation) wamezindua mfumo wa huduma mpya ya BIMA ambapo T-PESA anakuwa mshirika muhimu katika mfumo huo kwa upande wa malipo kwa wanufaika.

Bima hii inayotambulika kama Gracias Life, T-PESA ni daraja muhimu katika mfumo huo wa bima kwa kukusanya ada za wanachama na kulipa madai ya wanachama yakijitokeza.

Aidha huduma hii itawasaidia Wakuu wa Taasisi pamoja na familia zao endapo kutatokea janga lolote lile miongoni mwao hususan misiba pamoja na matatizo mbalimbali ya kijamii kama ilivyo lengo la Umoja wao.

Kupitia ushirikiano huu, T-PESA inalenga kupanua wigo wa upatikanaji wa watumiaji wa huduma za T-PESA na ni sehemu ya jitihada za kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha na za Bima na kuwakaribisha Wananchi kufurahia huduma hii.